Nandy Atangaza Tarehe Rasmi Atakayopeleka Nandy Festival Dar es Salaam

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Joto la burudani linazidi kuongezeka nchini Tanzania kwani mfumo umekuwa tamasha baaada ya tamasha. Siku chache tu baada ya Zuchu kujaza uwanja wa Imani mkoani Zanzibar kupitia tamasha la Zuchu Homecoming, mwenzake Nandy ametangaza tarehe rasmi ambayo tamasha lake la Nandy Festival litafanyika Dar es Salaam.

Soma Pia: Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy ametangaza kuwa atatua na tamasha lake Dar es Salaam mnamo tarehe nne mwezi wa tisa mwaka huu.

Maelezo kuhusiana na tamasha hilo hata hivyo bado yangali finyu kwani Nandy hakufichua ukumbi wa tamasha hilo au wasanii wengine ambao ataambatana nao.

Tayari Nandy amekwisha tumbuiza katika mikoa mbali mbali ikiwemo; Arusha, Zanzibar, Dodoma na Mwanza, na kwa sasa imwewadia zamu ya mashabiki wake walioko mkoani Dar es salaam kupata kipimo chao cha burudani.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Nimekuzoea’

Nandy amesifiwa mno na wadau mbali mbali katika sekta ya burudani Tanzania kutokana na mafanikio makubwa ambayo ameyapata kupitia tamasha la Nandy Festival ambalo yeye hufanya kila mwaka.

Nandy Festival huwaleta pamoja wasanii wakubwa kutoka ndani na nje ya Tanzania. Hapo awali Nandy aliwaleta wasanii kama vile Joeboy, mchekeshaji kutoka Kenya Jalang'o, msanii Tanasha Donna na wengine wengi kwa minajili ya kuwapa mashabiki wake burudani isiyo na kifani.

Leave your comment