Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Nimekuzoea’

[Picha: Buzz Central]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Nandy ameendelea kuimarisha himaya yake ya muziki kwa kutoa video ya wimbo wake wa ‘Nimekuzoea.

Video ya wimbo huo inaonekana kufanyika Afrika Kusini na kampuni ya Islanders imehusika katika shughuli hio.  

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Azungumzia Mahusiano ya Rayvanny, Harmonize na Jux Kwenye ‘New Couple’

Kwenye video ya ‘Nimekuzoea’, Nandy anachukua uhusika wa mwanafunzi wa kike ambaye yupo masomoni lakini anavutiwa sana kimapenzi na mwalimu wake wa darasani. Sambamba na hilo kwenye video hiyo, Nandy anaonesha uwezo wake wa kucheza kwani video hii ina miondoko tofauti tofauti.

Kupitia YouTube, mashabiki wengi wameonekana kuleta mrejesho chanya kuhusiana na video hii ambapo watu wengi wametoa maoni yao wakionesha kupenda kilichoonekana ndani ya video.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: EP 5 Mpya Zilizoachiwa Bongo Mwezi Juni 2021

"We've been waiting a lot. Tumedance sana," alichangia mtumiaji mmoja wa Youtub, huku  mwingine akiandika "Finally the most awaited video is out".

Ikumbukwe kuwa wimbo wa ‘Nimekuzoea’ ulitoka Tarehe 4 Juni mwaka huu na ni wimbo pia unaopatikana kwenye EP ya Nandy inayokwenda kwa Jina la ‘Taste’.

EP hio ina nyimbo nne kama vile; ‘Yuda’, ‘New Couple’ na ‘Yote sawa’. Hii ni video ya nne kutoka kwa Nandy mwaka 2021 kwani Januari 8 mwaka huu aliachia video ya ‘Number one’ akiwa pamoja na Joeboy, kisha Februari 26 akatoa video ya ‘Leo Leo’ aliyofanya na Koffi Olomide, kisha April 5 Nandy alitoa video ya ‘Wanibariki’ iliyoongozwa na Desro kutokea Wanene Filmz.

https://www.youtube.com/watch?v=3I05z8Aa1BU

Leave your comment