Nyimbo Mpya: Nandy Azungumzia Mahusiano ya Rayvanny, Harmonize na Jux Kwenye ‘New Couple’

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota wa Kitanzania Nandy hivi karibuni ameachia EP mpya kwa jina ‘Taste’ yenye  nyimbo nne.

Miongoni mwa nyimbo ambazo ziko kwenye EP ni pamoja na, ‘Nimekuzoea’, ‘Yote Sawa’, ‘New Couple’ na ‘Yuda’.

Soma Pia: Nandy Asafiri Nigeria, Atarajiwa Kuachia Kazi Mpya na Wasanii Wakubwa Naija

Nyimbo hizo zimekaribishwa vyema na mashabiki wake na wimbo uliotazamwa zaidi kati ya nne ikiwa ni 'Nimekuzoea' ambayo ilikuwa ya kwanza kutolewa.

Nandy anajulikana kwa kuimba juu ya mapenzi na nyimbo nne zinasimulia hadithi tofauti za mapenzi.

Katika wimbo wa ‘New Couple’, Nandy amewataja baadhi ya watu mashuhuri nchini Tanzania. Wimbo huo unazungumzia kuibuka kwa wanandoa wapya kila siku na jinsi uhusiano unamalizika licha ya watu kutumaini kwamba wangekaa kwa muda mrefu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Wimbo Mpya ‘Nimekuzoea’ Toka EP ya ‘Taste’

Nandy aliwataja baadhi ya wanandoa maarufu ambao walikuwa wamegonga vichwa vya habari kwa kupendana lakini mwishowe wakaachana. Anaanza wimbo kwa kutaja Venessa na Jux, Aslay na Tesi, Harmonize na Sarah, Rayvanny na Fayvanny kati ya wengine.

Pia alizungumza kuhusu uhusiano wake na Bilnass.

"Ningependa kumwona Vanessa an Jux, mara ikatokea nuksi tena wakatengana, Aslay zoea akamwona na Tesi ... hakutegemea kuona Harmo na Sarah wakiendelea, ila mambo yamebadilika kuona na Kajala, ila namwombea," Nandy aliimba.

https://www.youtube.com/watch?v=1veAMqS2VpY

Leave your comment