Harmonize Afichua Sababu Iliyomfanya Kuanzisha Lebo ya Konde Music Worldwide

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Harmonize amefunguka kuhusu kilichomsukuma kuanzisha lebo ya rekodi ya Konde Music Worldwide. Kwa sasa Konde Music Worldwide ni mojawapo ya lebo zenye mafanikio makubwa sana si Tanzania tu, bali Afrika Mashariki nzima.

Soma Pia: Harmonize Amshauri Ibraah Kuacha Ugomvi na Wasanii Wengine Bongo

Hapo awali, Harmonize alikuwa amesainiwa chini ya lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz. Alipata umaarufu wake kupitia WCB ila baadaye akaondoka kwenye lebo hiyo.

Kwenye chapisho alililoliandika mtandaoni, Harmonize alidai kuwa alitaka kujisimamia kimuziki. Alieleza zaidi kuwa pia ilikuwa ndoto yake kumiliki lebo. Kilicho anza kama wazo na ndoto hatimaye kilitendeka na kupata mafanikio.

Harmonize ambaye pia anajulikana kama Tembo katika usanii, aliwashukuru mashabiki kwa kumonyesha upendo na vilevile kumuunga yeye pamoja na wasanii waliopo kwenye lebo yake mkono.

Soma Pia:Harmonize Amtaja Ibraah Kama Mfalme wa Muziki wa Kizazi Kipya

Alikiri kuwa wakati anaanzisha lebo hakuwa na pesa za kutosha ambazo angeekeza kwa msanii, ila kupitia upendo wa mashabiki wake, hatimaye wasanii kwenye lebo hiyo walipata umaarufu pia.

"Ilianza kama ndoto ikawa wazo ..!! Kufungua record label lengo ni kujisimamia mwenyewe na kazi zangu za muziki lakini upendo mulionionyesha ulinipa nguvu ya kushika wengine mikono kwa pamoja tuzikimbilie ndoto zetu hasa sisi vijana wa kimaskini licha ya kwamba sikuwa na hela zakumfanya msaniii akawa maarufu lakini niliamini sana kupitia upendo wenu ambao unazidi pesa zote dunianii," Harmonize alisema.

Harmonize kwa sasa ni mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika na mwenye wafuasi wengi katika mitandao mbali mbali ya kijamii.

Leave your comment