Harmonize Amshauri Ibraah Kuacha Ugomvi na Wasanii Wengine Bongo

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amemshauri msanii Ibraah kusuluhisha tofauti zake na wasanii wengine katika tasnia ya muziki ya Bongo.

Soma Pia: Harmonize Amtaja Ibraah Kama Mfalme wa Muziki wa Kizazi Kipya

Harmonize katika ujumbe aliouchapisha mtandaoni, alisema kuwa hafurahii kumwona Ibraah akiwa na ugomvi na wanamuziki wenzake. Harmonize alieleza kuwa wasanii wanategemewa na jamii kuipeperusha bendera ya Tanzania na hivyo basi sio picha nzuri kuwaona wakigombana hadharani.

Msanii huyo ambaye pia ni bosi wa Ibraah aliongeza kuwa yeye binafsi hakuwa amependezwa.

Maneneo ya Harmonize yalitokana na chapisho ambalo Ibraah alikuwa ameeka mtandaoni. Kwenye chapisho hilo Ibraah alionekana kumuingilia msanii mwenzake ambaye hakumtaja kwa jina.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo na Wasanii Diamond, Rayvanny, Zuchu na Ibraah

Ibraah alijisifia kwa kusema kuwa yeye alikuwa mchanga ila mwerevu sana.

“Lecturer somo limemshindwa! Vumbi tu, I am young and genius," chapisho la Ibraah lilisomeka.

Harmonize alimjibu Ibraah kwenye sehemu ya maoni ya chapisho hilo.

"Kwa faida ya sanaa ya Tanzania na vizazi vijavyo nisingependa kuona mkigombana naamini wote ni vijana na mna ndoto isitoshe family's zinawategemea fanya muyamalize matatizo yenu. Binafsi sipendezwi kila mtanzania halisi anawategemea kesho je kuipeperusha hii bendera," Harmonize alisema.

Ujumbe wa Harmonize uliibua hisia tofauti huku wengi wakimsifu kwa busara alioonyesha katika kumshauri Ibraah.

Ibraah katika mahojiano ya hivi karibuni alijitokeza na kukana madai kuwa ako na uhasama na wasanii wenzake. Aliweka wazi na kusistiza kuwa yeye hana ugomvi na msanii yoyote nchni Tanzania.

Leave your comment