Harmonize Amtaja Ibraah Kama Mfalme wa Muziki wa Kizazi Kipya

[Picha: Capital FM]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu Harmonize amemtaja msanii Ibraah aliyesainiwa katika lebo yake ya Konde Music Worldwide kama mfalme wa muziki wa kizazi kipya. Katika chapisho aliloliandika, Harmonize alidai kuwa alikuwa ameona nyota hiyo ndani yake Ibraah kabla ata ya yeye kupanda ngazi na kufikia alipo leo kimuziki.

Soma Pia: Wimbo Mpya wa Ibraah 'Jipinde' Wamuandikishia Rekodi Mpya

Harmonize aliambatanisha chapisho hilo pamoja na picha iliyoonyesha jinsi wimbo mpya wa Ibraah uitwao 'Jipinde' ulikuwa umepata watazamaji taakriban milioni moja nukta tisa.

Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldiwide alimpongeza Ibraah kutokana na mafanikio ambayo ngoma yake mpya ilikuwa imepata. Alisema kuwa alikuwa amepndezwa na kazi ya Ibraah.

"Congrats big brother @ibraah_tz day one I told you, you are the king of new school wachache hawakunielewa proud of you Chinga," Harmonize alisema katika chapisho lake.

Soma Pia: Ibraah Ajibu Madai ya Kununua Watazamaji wa Wimbo wake ‘Jipinde’ Kwenye YouTube

Hapo awali katika chapisho tofauti, Harmonize alidai kuwa Ibraah amepitia changamoto mingi kimuziki na licha ya hayo yote, ameibuka na kuwa mwenye mafanikio makubwa. Kulingana na Harmonize, wapo waliojaribu kukatisha ndoto ya Ibraah katika muzikilakini hawajafaulu.

Kwa sasa, Ibraah anatamba katika anga za burudani za Afrika Mashariki kupitia ngoma yake mpya 'Jipinde'.

Ngoma hiyo imeandikisha rekodi kwa kuwa wimbo wa kwanza wa Ibraah kupata watazamaji wengi sana nadani ya muda mfupi.

Ibraah ni mmoja wa wasanii chipukizi nchini Tanzania ambao wamekuwa kwa kasi sana na kupata umaarufu pamoja na mafanikio.

Leave your comment