Nyimbo Mpya : Maud Elka Amshirikisha Alikiba Kwenye Songi Songi Remix

[Picha: Songi Songi Video YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea Congo Maud Elka ameachia remix ya wimbo wake "Songi Songi" akiwa amemshirikisha Alikiba.

Toleo halisi la wimbo huu ilitoka Machi mwaka huu ambapo Maud Elka alimshirikisha msanii Hiro pia kutokea nchini Congo na wimbo huo uliweza kufanya vizuri sana barani Afrika na hata nchini Tanzania.

Kwenye remix ya wimbo huu, msanii Alikiba ameweza kuimba kwa ufasaha lugha ya kifaransa huku akiongeza na maneno machache ya Kiswahili kunogesha zaidi wimbo huo.

Soma Pia: Alikiba Asifia Ustadi wa Diamond Katika Kutunga Wimbo wa 'Kamata'

Alikiba anajulikana kwa uwezo wake wa kuweza kuimba kwa lugha ya kifaransa kwani kwenye wimbo wake wa ‘Aje’ alioutoa mwaka 2016 kwenye aya ya pili aliimba kwa lugha ya Kifaransa kwa ufasaha sana.

"Nipatavyo kwako kwingine sijaona na ukiniumiza majeraha majeraha sitapona unausonga kama dona baby waona waona nausikiliza unanitatiza we ukiniacha mbali mi utaniliza," anaimba msanii Alikiba kwenye aya ya pili ya wimbo huu.

‘Songi Songi’ remix imeandaliwa na Narco Vera Beats pamoja na Fabio Litto kutokea. nchini Ufaransa.

Soma Pia: Madai ya Ununuzi wa Watazamaji Yaibuka Baada ya Diamond, Alikiba Kuachia Nyimbo Zikifuatana

Kufikia sasa ‘Singo Singo’ remix imeshatazamwa mara laki moja na sabini kwenye mtandao wa YouTube.

Maudi Elka ni nani?

Maudi Elka ni mwanamuziki anayeimba kwa lugha ya kifaransa mwenye asili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Mwaka 2013 Maudi alitamba baada ya kutoa wimbo wa ‘Buzz l'éclair au chocolat’ akishirikiana na rapa Dino. Ilipofika mwaka 2018 baada ya kushinda shindano la muziki alipata nafasi ya kutumbuiza na wasanii kama Dadju na Vegedream.

Ilipofika Machi 2019, alitoa EP yake ya kwanza chini ya Lebo ya Spinup inayoitwa PQM iliyosheheni nyimbo sita ambazo nyingi zimesheheni vionjo vya muziki wa Pop.

https://www.youtube.com/watch?v=X1-vDQIrBCU

Leave your comment