Sitawaangusha: Zuchu Awashukuru Mashabiki Kwa Kumuunga Mkono

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika Zuchu kutokea lebo ya WCB amekuwa mwingi mwenye hisia kutokana na uungaji mkono ambao amepokea kutoka kwa mashabiki wake hivi karibuni. Zuchu yumo mbioni kufanikisha tamasha lake la kwanza kama mwanamuziki litakalofanyika tarehe 21 mwezi huu.

Soma Pia: Nyimbo 5 Ambazo Diamond Platnumz Ameshirikisha Wasanii wa Kike

Licha ya kuwa hili ndilo tamsha lake la kwanza, Zuchu amepokea uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Katika ujumbe tofauti alizochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Zuchu aliwashukuru wale ambao wamejitokeza na kumuunga mkono au kuchangia katika kufanikisha tamasha lake la Zuchu Homecoming kwa njia yoyote ile.

Katika chapisho la hivi karibuni, Zuchu aliwashukuru wafuasi wake kutoka Zanzibar ambao walijitokeza kununua tiketi na pia kupiga kampeni ya kufanikisha tamasha hilo. Aidha Zuchu aliwaahidi mashabiki wake kuwa hatawafeli katika kutoa burudani siku hiyo kuu itakapowadia.

Soma Pia: Zuchu Aomba Kuongezewa Ulinzi Kabla ya Kuachia Ngoma Mpya

Ni muhimu pia kukumbuka kuwa kwa heshima aliyonayo Zuchu kwa mashabiki wake, aliamua kufanya tamasha lake la kwanza mkoani Zanzibar alikozaliwa na kukuzwa.

"Hii video nimeangalia nimefurahi mpaka nimelia. Mtaani kwetu kwaalinato waliposikia ticket zimefika wakaomba team ya Wasafi Iwapelekee .Wallahi I’M So Happy Kwa jinsi Mnavyonipendelea na kunipigania Napokea Simu Nyingi Kila Mtu Ananambia tunakuunga mkono. Haki ya Mungu hata muwe wachache vipi ilimradi unanisupport nasema hiyo support ni kubwa kuliko unavyoweza kudhani na kwa mnavonishikilia nasema asante na sitowaangusha," ujumbe wa Zuchu mtandanoni ulisomeka.

Leave your comment