Zuchu Aomba Kuongezewa Ulinzi Kabla ya Kuachia Ngoma Mpya

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka lebo ya WCB Zuchu amewashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza kuwa anahitaji ulinzi zaidi kabla ya kuachia wimbo wake mpya.

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

Zuchu alichapisha taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram, huku akisisitiza kuwa ngoma hiyo huenda ikahatarisha maisha yake.

Zuchu hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu taarifa yake. Japo hakusema tarehe kamili atakayoachia ngoma hiyo inayoonekana kukumbwa na utata, Zuchu aliahidi kuwa tarehe 21 mwezi huu katika tamasha yake ya Zuchu Homecoming kuwa patajaa pomoni.

"Goma naloenda kuachia naomba kuongezewa ulinzi aki vile linaeza kuhatarisha maisha yangu. Tarehe 21/08/2021 patakua hapatoshi," Ujumbe wa Zuchu ulisomeka.

Soma Pia:  Zuchu Asimulia Alivyokaribia Kuacha Muziki Akiwa WCB

Zuchu kwa sasa yumo mbioni kufanikisha tamasha lake la Zuchu Homecoming litakalo fanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar. Hili ndilo litakalokuwa tamasha la kwanza la msanii huyo ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa takriban mwaka mmoja sasa.

Zuchu alipata mafanikio makubwa sana kwenye taaluma yake ya muziki katika muda mfupi, na ni msanii ambaye amekua kwa kasi mno. Katika mahojiano ya hivi karibuni na mwanahabari wa Kenya Mzazi Wlly M Tuva, Zuchu alieleza kuwa mafanikio yake yalitokana na yeye kuwa katika lebo ya WCB.

Alifichua kuwa mikakati na taratibu zimeekwa katika lebo hiyo kusudi kuhakikisha kuwa kila msanii anafanya kazi kwa bidii. Zuchu kwa sasa bado anatamba katika anga za burudani na ngoma yake ya ‘Nyumba Ndogo’.

Leave your comment