Nandy Awashukuru Wasanii Waliodhuria Hafla Ya Kuskiza EP Yake Mpya ‘Taste’

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pakua Nyimbo Zake Nandy Bure Kwenye Mdundo

Msanii Nandy amechapisha mtandaoni ujumbe wa shukrani kwa mastaa wote waliotii mwaliko wa kuskiza Taste EP yake. Msanii huyo alikuwa na hafla ya usikilizaji wa Taste EP ila hafla hiyo ilihudhuriwa na watu walioalikwa tu.

Soma Pia: Nandy Atangaza Kolabo Mpya Na Sho Madjozi

Wengi waliodhuria hafla hiyo walikuwa wasanii na mastaa wengine mbali mbali kwenye tasnia ya burudani ya Tanzania. Nandy aliimba nyimbo zote nne zilizopo kwenye Taste EP ambayo aliachia hivi majuzi.

Nyimbo zote zilizoko kwenye Taste EP hiyo zilipata mafanikio huku nyimbo iliyovuma zaidi ikiwa 'Nimekuzoea'.

Katika video ambayo Nandy alichapisha mtandaoni, alionekana akizungumza na wasanii wenzake mbali mbali. Baadhi ya wasanii walionekana wakiwa katika mazungumzo na Nandy ni Darassa na Ben Pol. Aidha Nandy pia alishukuru vyombo vya habari ambavuo vilihudhuria hafla yake.

Soma Pia: Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

"Asanteni wote mliokuja kufurahia na mimi usiku wa juzi! Media zote makampuni yote wasanii ndugu na marafiki shukrani za dhati sana sana," ujumbe wa Nandy katika ukurasa wake wa Instagram ulisomeka.

Nandy amesifiwa na wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki kama mmoja wa wasanii wa kike wanaojituma sana. Hapo awali msanii tajika kutoka Tanzania Alikiba alisema kuwa Nandy ni msanii mwenye bidii ambaye amepanda ngazi na kusimama imara katika tasnia iliyojawa na wanamuziki wa kiume.

Alikiba katika ujumbe huo aliwaomba watanzania kuwaunga mkono zaidi wasanii wa kike.

Leave your comment