Mayorkun Ampongeza Alikiba Baada ya ‘Jealous’ Kufanya Vizuri

[Picha: Jealous Video YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Nigeria ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo wa ‘Jealous’ wa Alikiba Adewale Mayowa Emmanuel almaarufu kama Mayorkun amempongeza King Kiba kutokana na wimbo huo kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Madai ya Ununuzi wa Watazamaji Yaibuka Baada ya Diamond, Alikiba Kuachia Nyimbo Zikifuatana

Kupitia akaunti yake ya Instagram sehemu ya Instastory, Mayorkun alionekana kushangazwa na wimbo huo kufanya vizuri ndani ya muda fupi na kumpongeza Alikiba kwa hatua hiyo.

"5 Million that was quick congrats Broski Alikiba," aliandika Mayorkun.

Kufikia sasa, video ya ‘Jealous’ iliyofanyika nchini Nigeria chini ya director Dayamund imeshatazamwa mara milioni tano nukta mbili kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ni siku sita tu tangu kuachia kwake na kwa sasa ni video namba mbili kwenye orodha ya video zinazotamba sana kwenye mtandao huo nchini Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Jealous’ Akimshirikisha Mayorkun

Aidha, video hii ilitengeneza rekodi ya kutazamwa mara milioni moja ndani ya masaa 12 na hii ilifanya video hii kuongekewa sana kwenye mtandao huo. Kwa mwaka huu pekee, msanii Alikiba ameshatoa video nne ya kwanza ikiwa ni "Infedele" iliyotoka Januari, ikifuatiwa na "Ndombolo" na "Salute" zilizotoka mwezi Juni na hii ya "Jealous" iliyotoka mwezi Julai mwaka huu.

Aidha Alikiba mara kwa mara kupitia mahojiano yake kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii amekuwa akidokeza kuwa yuko mbioni kutoa albamu na mfululizo huu wa kutoa video ni maandalizi ya albamu hiyo kutoka kwa Alikiba.

https://www.youtube.com/watch?v=LQyCY1t--GU

Leave your comment