Zuchu Afichua Idadi ya Nyimbo Alizorekodi Ndani ya Wiki Moja

[Picha: Zuchu Facebook]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka WCB Zuchu amewaacha mashabiki wake na hamu baada ya kufichua kuwa hivi karibuni alirekodi nyimbo saba ndani ya wiki moja.

Katika taarifa aliyochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Zuchu aliambatanisha taarifa hiyo pamoja na video iliyomwonyesha akiwa studioni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Sweet’ Akimshirikisha Guchi

Kilichowafurahisha mashabiki zaidi ni kuwa nyimbo hizi zilikuwa zimeimbwa katika lugha tofauti. Zuchu, hata hivyo, hakupeana maelezo zaidi haswaa kuhusu majina ya nyimbo hizo wala lugha alizozitumia.

Zuchu ni msanii anayejulikana kwa uwezo wake wa kupitisha ujumbe kupitia sauti yake tamu na hisia nzito haswaa inapokuwa nyimbo ya mapenzi. Japo hajasema, inatarajiwa kuwa angalau katika nyimbo hizo patakuwepo na wimbo wa mahaba.

Soma Pia: Nyimbo Tano Bora za Amapiano Zilizoachiwa na Wasanii Kutoka Bongo

Video aliyochapisha pia ilitoa matumaini ya wimbo wa mahaba kwani kwenye video hiyo fupi Zuchu aliskika akiimba wimbo wa mapenzi.

"Nimerecord Zaidi ya Nyimbo 7 Ndani ya wiki za lugha Tofauti Tofauti This one was a freestyle from yesterday’s Session With @iam_trone FIRE," Zuchu aliposti.

Zuchu kwa sasa amepanda ngazi na kuwa mmoja wa wasanii wanaotamba sana kwenye anga za burudani Tanzania. Hii ni licha ya kuwa mwanamuziki huyo amekuwa katika tasnia ya muziki kwa takriban mwaka mmoja tu.

Zuchu hivi karibuni aliachia wimbo wake wa ‘Nyumba Ndogo’ ambayo ilipokelewa vizuri sana. Aidha, Zuchu yupo kwenye harakati za kufanikisha tamasha lake la Zuchu Homecoming litakalofanyika tarehe 21 mwezi Agosti katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Leave your comment