Alikiba Ahairisha Kutoa Video ya 'Jealous' Baada ya Kifo Cha Malcom Ally

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Alikiba ametangaza kuairisha kutolewa kwa video yake mpya ‘Jealous’ baada ya kifo cha rafiki yake Malcolm Ally.

Hapo awali, Alikiba alikuwa ametangaza kuwa attachia video hiyo hii leo tarehe 29 mwezi Julai. Hamu iliongezeka ata zaidi pale Diamond Platnumz ambaye ni mpinzani mkuu wa Alikiba alitangaza kuwa pia attachia video ya wimbo wake wa ‘Iyo’ siku hiyo hiyo.

Soma Pia: Yogo Beats Afunguka Kufanya Kazi na RudeBoy Kwenye ‘Salute’ya Alikiba

Wengi walisubiri sana huku wakitarajia kuwa kivumbi kitatamba na gwiji wa bongo kutambulika. Hata hivyo Alikiba baadae alijitokeza na kutangaza kuhairishwa kwa video ya wimbo wa ‘Jealous’.

 Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa Twitter, Alikiba alieleza kuwa alilazimika kuhairisha video hiyo kwa sababu ya kifo cha Malcom Ally ambaye alikuwa rafiki wake wa karibu sana.

Video ya wimbo wa Jealous kwa sasa inatarajiwa kuachiwa rasmi mnamo Ijumaa tarehe 30 mwezi julai mida ya saa tano asubuhi.

Soma Pia: Alikiba Asifia Ustadi wa Diamond Katika Kutunga Wimbo wa 'Kamata'

"Owing to the unfortunate demise of my dear friend Malcom Ally Masoud, I have decided to postpone the release of the music video for “Jealous” until 11 am on Friday, 30th July," Chapisho la Alikiba lilisoma.

Hapo awali Alikiba alituma rambirambi zake kwa familia ya Malcom Ally na kuwaombea kuwa na nguvu wakati huu mgumu wa kifo cha Malcom Ally.

Leave your comment