Nyimbo Mpya: Diamond Aachia Video ya ‘Iyo’ Akiwashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazzi

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Diamond Platnumz ametoa video ya wimbo wake wa ‘Iyo’ aliowashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazzi.

Video hiyo imeongozwa na Hanscana ambaye ni mojawapo ya waongoza video bora nchini Tanzania. Hii ni mara ya pili kwa Diamond Platnumz kufanya kazi na Hanscana kwani wawili hao walishafanya kazi kwenye video ya ‘Nasema Nawe’ iliyotoka Machi 27 mwaka 2015.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano 5 Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Wengi wanaomfahamu Diamond Platnumz hukiri msanii huyu hana shughuli ndogo, na bila shaka ameendeleza kasumba hiyo kwenye video hii ambayo imefanyika kwenye mandhari ya uswahilini yanayoakisi maisha halisi ya watanzania walio wengi.

Aidha, video hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho imepambwa na miondoko tofauti tofauti ya dansi kiasi cha kuifanya video hii kuchangamka vilivyo lakini pia kitendo cha Hanscana kutumia watu wa rika mbalimbali kama watoto wa shule kwenye video imefanya ‘Iyo’ iwe ni mali na turufu kwa watu wa rika zote.

Soma Pia: Diamond Avimba Baada ya Wimbo wake 'Iyo' Kuvuma Afrika Kusini

Upande wa YouTube kufikia sasa watu takribani elfu tano wametoa maoni yao kuhusiana na video hii huku watu ishirini na mbili elfu wakipenda video.

Kupitia mtandao wa YouTube video ya ‘Iyo’ imetengeneza rekodi ya kipekee kwani ndani ya dakika ya 38 tangu video hiyo itoke ilitazamwa mara laki 100,000 na hii inafanya msanii Diamond platnumz kuvunja rekodi yake mwenyewe kwani kwenye video ya "Waah" ilitazamwa mara 100,000 ndani ya dakika 48.

https://www.youtube.com/watch?v=UcOSSs3CNQ0

Leave your comment