Makamu wa Rais wa Zanzibar Abariki Tamasha la Zuchu Homecoming

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka lebo ya WCB Zuchu kwa sasa yuko mbioni kufanikisha tamasha lake la Zuchu Homecoming litakalofanyika tarehe 21 mwezi Agosti katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Soma Pia: Zuchu Apongeza Serikali ya Tanzania Kwa Kuendeleza Sanaa ya Muziki

Zuchu alizaliwa na kulelewa Zanzibar na hivyo basi Tamasha hilo litakuwa njia mwafaka ya yeye kutoa shukrani kwa mashabiki wake waliomwona akiwa bado mchanga kimuziki. Zuchu pia ametua tamasha hiyo kuwajenga wasanii chipukizi kwa kuwapea fursa ya kutumbuiza jukwaani na pia kuelimishwa zaidi kuhusu masuala ya kimuziki.

Hivi karibuni Zuchu alikutana na makamu wa rais wa Zanzibar Hemedi Suleiman Abdulla na kujadili mambo mbali mbali kuhusu tamasha la Zuchu.

Kulingana na taarifa ambayo Zuchu alichapisha mitandaoni, Mheshimiwa Hemedi alilibariki Tamasha la Zuchu Homecoming. Aidha Zuchu alimshukuru kiongozi huyo kwa kukubali kushiriki katika maandalizi ya tamasha hilo.

Soma Pia: Kongamano La Zuchu Lapata Mafanikio Makubwa Zanzibar

"Ahsante sana mheshimiwa makamu wa raisi Hemed Suleiman kwa baraka zako @ofisi_makamu_wa_pili .Tulizungumza mengi na naahidi kuyafanyia kazi .Na nishuru kwa mapokezi na support mliuitupa. Nashukuru sana mheshimiwa. Tarehe yetu ni 21/08/2021 uwanja wa amani," Zuchu aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Zuchu pia alieleza kuwa tamasha hilo litang'oa nanga saa saba mchana kusudi kuwaruhusu watoto pia wahudhurie.

"Milango itakua wazi kuanzia asubuhi saa 1:00 na show itaanza saa 7 mchana ili tuweze kuwapa nafasi na watoto nao waweze kuburudika," Zuchu alitangaza.

Hapo awali, Zuchu katika mahojiano na Wasafi TV aliwasifu viongozi wa serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono ukuzi wa sanaa ya muziki.

Leave your comment