Zuchu Apongeza Serikali ya Tanzania Kwa Kuendeleza Sanaa ya Muziki

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka lebo ya WCB Zuchu amepongeza na pia kutoa shukurani kwa serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono ukuaji wa sanaa ya muziki. Akizungumza katika kongamano lake lililofanyika Zanzibar, Zuchu alieleza kuwa serikali kupitia viongozi mbali mbali ilikuwa imehusika pakubwa katika kufanikisha tamasha lake la Zuchu Homecoming.

Soma Pia: Kongamano La Zuchu Lapata Mafanikio Makubwa Zanzibar

Zuchu alitoa mifano kadhaa ya jinsi walivyolazimika kutiisha usaidizi ya mawaziri kadhaa kusudi kufanikisha miradi mbali mbali. Alisema kuwa wakati mwingine yeye pamoja na timu yake hulazimika kuwaamsha viongozi usiku wa manane wanapokumbwa na jambo la dhararu katika kuandaa tamasha.

Alisema kuwa Waziri wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita alimshika mkono sana alipotoa wazo la kufanya tamasha la Zuchu Homecoming.

Soma Pia: Diamond Platnumz na Rayvanny Wadokeza Ujio wa Wimbo Wao Mpya

"Hii inaonyesha kwamba tuna viongozi ambao wanajali na wanapenda maendeleo na ukuaji wa tasnia zetu. Acha nikupe mfano, wakati naenda kwa mheshimwa Leila kumpa idea ya kwamba nataka kujaza uwanja, akaniambia utajaza na mimi nitakusaidia," Zuchu alisema.

"Tuseme kila kampeni tunayoiandaa kwenye hii show, mheshimiwa waziri Tabia ametusupport kwa asilimia kubwa. Tunampigia simu hadi usiku sometimes kutaka vitu hadi protocal zivunjwe anatusaidia. Kwa hivyo niseme wasanii wa Zanzibar tutumie hii fursa vizuri," Zuchu aliongezea.

Tamasha la Zuchu Homecoming linatarajiwa kufanyika mwezi ujao katika uwanja wa Amani, Zanzibar. Tamasha hilo litakuwa kubwa na la aina yake kwani wasanii chipukizi kutoka Zanzibar watakuwepo jukwaani kutumbuiza.

Leave your comment

Top stories