Kongamano La Zuchu Lapata Mafanikio Makubwa Zanzibar

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwimbaji maarafu kutoka Bongo Zuchu amejitokeza kuelezea furaha yake baada ya kongamano aliloliandaa kule Zanzibar kupata mafanikio makubwa sana. Kongamano hilo la Zuchu lililofanyika wikendi lilikusudia kuwaleta wasanii chipukizi pamoja na kuwaelemisha zaidi kuhusu sanaa ya muziki.

Soma Pia: Diamond Platnumz na Rayvanny Wadokeza Ujio wa Wimbo Wao Mpya

Katika mahojiano na Wasafi TV, Zuchu alisema kuwa alishangazwa na jinsi watu walivyojitokeza kwa idadi kubwa kusudi kuhudhuria kongamano hilo. Kulingana na Zuchu, hakudhani kuwa Zanzibar ilikuwa imewabeba wasanii wengi hivyo wenye talanta za kuvutia.

Aidha, Zuchu aliongezea kuwa kongamano hilo lilikuwa mojawapo ya maandalizi ya tamasha la ‘Zuchu Homecoming’ litakalofanyika mnamo tarehe 21 mwezi Agosti katika uwanja wa Amani.

"Kwanza jana waliponiambia kuwa wataeka viti mia mbili, sikutegemea kwamba watu watajaa. Mimi mwenyewe ata sikujua kuwa Zanzibar tuna wasanii mia mbili. Kwa hivyo niseme kuwa nimefurahi, na sijafurahi juu yangu, nimefurahi kwa sababu huu mwitiko unaonyesha kwamba wasanii wa Zanzibar wana kiu ya kutaka kuinuka.

Soma Pia: Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

“Mwanzo nilisema, dhumuni ya kongamano hili, sio ati tunaenda kuwafundisha watu hawajui, hapana, ni kuenda kuwapa watu njia ya kuendelea kujiinua," Zuchu alisema.

Msanii huyo kutoka WCB pia alifichua kuwa wasanii chipukizi watachaguliwa kutoka kwa kongamano hilo ili waende kutumbuiza katika tamasha la ‘Zuchu Homecoming’.

Zuchu aliwashauri wale watakao pata fursa hiyo kuitumia vizuri na kuonyehsa dunia talanta zao pasi na kufikiria anatazamwa na nani.

Leave your comment

Top stories