Country Wizzy na Ibraah Kuja na Wimbo Mpya wa Pamoja

[Picha: Countrywizzy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na bila shaka nyota kutokea Konde Gang Country Wizzy na Ibraah wamedhihirisha hilo baada ya kuonesha dalili ya kuachia ngoma ya pamoja. 

Country Wizzy alichapisha video kupitia akaunti yake ya Instagram ikiwaonesha Ibraah na Wizzy wakiwa wanafurahi studio na mtayarishaji wa muziki Bboy Beats akiwa pembeni huku mdundo wa nyimbo hiyo ukisikika kwa mbali. 

"They are not ready for this" alisikika Country Wizzy akisema kwenye video akimaanisha mashabiki bado hawapo tayari kusikia wimbo huo. 

Soma pia: Harmonize Afafanua Dhamira ya Kuachia wimbo wa ‘Sorry’

Kama wimbo huu utakuwa tayari itakuwa ni mara ya kwanza kwa Country Boy na Ibraah kusikika kwenye wimbo mmoja na bila shaka mashabiki watakuwa na hamu sana kusikiliza wimbo huo. 

Kwa sasa msanii Country Wizzy anatamba na wimbo wake wa "Hiphop" aliouachia Julai 4 mwaka huu na kufikia sasa video ya wimbo huo imetazamwa mara laki moja sitini na mbili kwenye mtandao wa Youtube. 

Kwa upande wa Ibraah alitoa wimbo wake wa mwisho "Hayakuhusu" wimbo ambao ulizua taharuki sana kutokana na mashairi yake lakini Mei 30 alishirikiana na Kinata Mc kwenye "Do Lemi Go".

Soma pia: Lulu Diva Apongeza Singeli ya Hamisa, Atangaza Ujio wa Albamu mpya

Wasanii wote wawili Ibraah na Country Wizzy wako chini ya Konde Music Worldwide inayoongozwa na mwanamuziki  Harmonize na wote wawili pia wametangaza kwa wako mbioni kuachia albam.

Leave your comment