Harmonize Afafanua Dhamira ya Kuachia wimbo wa ‘Sorry’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Harmonize hatimaye amefunguka na kuelezea lengo  kuu la kuachia wimbo wa ‘Sorry.’ Ngoma hiyo ya Harmonize imevuma  na kuzagaa mtandaoni tangu kuchapishwa katika mtandao wa Instagram. Wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki walijitokeza na kumsifia Harmonize kwa kuimba kwa ustadi.

Soma Pia: Video 5 Zilizo na Watazamaji Wengi Zaidi YouTube Tanzania

Katika ngoma ya Sorry iliyotawaliwa na hisia nzito, Harmonize aliomba msamaha kwa mpenzi wake wa zamani Sarah. Msanii huyo  kupitia mistari ya wimbo wake alieleza kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwenye makosa na hakumwonyesha mpenzi wake upendo na heshima inavyostahili.

Ujasiri wa Harmonize wa kuomba msamaha hadharani pasi na kuogopa maneno atakayotupiwa mtandaoni na wakosoaji wake uliwapendeza watu wengi sana.

Soma pia:Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous'

Sarah kwa upande wake alijitokeza na kusema kuwa Harmonize alikuwa ametenda jambo la busara kwa kuomba msamaha. Sarah, hata hivyo, hakueleza iwapo amemsamehe au la.

Wengi walidhani kuwa kwa kuomba msamaha, Harmonize alitaka kurudiana na Sarah. Harmonize katika ujumbe aliochapisha mtandaoni alieleza kuwa lengo lake kuu la kuomba msamaha lilikuwa kuhakikisha kuwa kuna amani baina yake na Sarah.

Alikana madai ya kutaka kurudiana na Sarah na kusema kuwa kwa sasa hana nia ya kuingia katika mahusiano ya mapenzi na yeyote. Alisistiza kuwa kwa sasa anataka kukua pekee yake kwa muda.

"Sihitaji mahusiano mapya au ya zamani, I just made things clear and to appreciate the woman who was there for me tukapitia mengi, kuachana sio vita. Single forever," Chapisho la Harmonize lilisoma.

 

Leave your comment