Lulu Diva Apongeza Singeli ya Hamisa, Atangaza Ujio wa Albamu mpya

[Picha: Lulu Diva, BBC]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Lulu Diva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa "Samahani" akimshirikisha nyota kutokea WCB Lavalava, amempongeza msanii mwenzie Hamisa Mobeto baada ya wimbo wake wa "Ex wangu Remix"  kufanya vizuri. 

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha Wasafi Lulu Diva amempongeza Hamisa kwa kubadilika na kufanya muziki wa singeli ambao una ushawishi mkubwa sana hapa Tanzania. 

Soma pia:Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous'

Akiongelea, wimbo huo wa Hamisa, Lulu Diva alisema "Hamisa ametoa ngoma kali sana ni nzuri amebadilika nimependa. Nimependa alichokifanya Hamisa ametoa ngoma nzuri sina comment nyingi zaidi. Lakini its good i like it. 

Pongezi hizi kutoka kwa Lulu Diva zinakuja kipindi ambacho wimbo wa" Ex Wangu" unatamba sana hapa nchini Tanzania na hata kupitia mtandao wa Youtube ambapo kufikia sasa video ya wimbo imetazamwa mara Milioni 1 nukta nane kwenye mtandao wa Youtube ndani ya wiki wiki mbili tu. 

Kwa siku za hivi karibuni wasanii wengi wa bongo fleva kama Bright, Nedy Music, Zuchu, Ibraah na wengine wengi waliamua kutoa nyimbo za singeli na kupitia mahojiano hayo Lulu Diva aliweka wazi kuwa haoni hatari kufanya muziki wa singeli kwani ni aina ya muziki ambao unapendwa sana kwa sasa. 

"Kama itafika wakati nahitaji kutoa singeli nitafanya why not? Kwanini nisifanye singeli wakati najua kwamba ni mziki mzuri?" alizungumza msanii huyo. 

Sambamba na hilo Lulu Diva ameweka wazi kuwa anatarajia kutoa albamu mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2022.

"Nataka kuachia ngoma back to back sasa hivi lakini pia nina plan ya kuachia albam, nadhani mwezi wa 12 kama nitachelewa itakuwa Januari or Frebruari ila natamani watu waanze kupreorder kwanzia mwezi wa 12" alisema msanii huyo.

Leave your comment