Alikiba Atangaza Ujio wa Wimbo Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Alikiba ametangaza ujio wa nyimbo wake mpya hivi karibuni. Katika chapisho alilolieka kwenye mitandao ya kijamii, Alikiba ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa King's Music alifichua mada kuu katika wimbo wake ujao.

Ngoma ijayo ya Alikiba imepewa jina la ‘Jealous’, kwa maana ya wivu katika lugha ya Kiswahili. Mada kuu katika wimbo huo ni jinsi wivu inavyoathiri hali ya mapenzi baina ya watu wawili wanaopendana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Rudeboy Waachia Wimbo Mpya 'Salute'

Aidha Alikiba aliiwauliza mashabiki wake katika chapisho hilo iwapo washawahi kuhisi wivu katika hali yoyote ile. Msanii huyo alizidi na kuwaomba watumiaji wa mitandao ya kijamii kumfwata katika mitandao zake mbali mbali. Inatarajiwa kuwa bonge hilo la ngoma litatoka mwezi huu wa Julai japo kuwa bado tarehe kamili haijulikani.

"Before we continue with ‘Bampa To Bampa’ season, let me ask you ulishawahi kujiskia JEALOUS?? Kwenye kitu chochote? Subscribe to all of my digital platform channels," Ujumbe wa Alikiba uliochapishwa katika mtandao wa Instagram ulisoma.

Soma Pia: Alikiba Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kwa Albamu Yake

Alikiba kwa sasa yupo kwenye harakati ya kuachia nyimbo mfululizo bila ya kuwapea mashabaki nafasi ya kupumua. Alianza na wimbo wa ‘Ndombolo’ alioutoa kwa ushiriakiano na wasanii kutaka lebo yake ya King's Music. Kisha ikafuatiwa ‘Salute’ aliyoitayarisha kwa ushirikiano na msanii Rude Boy kutoka Nigeria. Nyimbo hizo mbili zilipokelewa vyema na mashabiki na zote kuvuma mtandaoni licha ya kuachiwa kwa ukaribu mno.

Leave your comment