Alikiba aachia kionjo cha wimbo mpya wa Injili [Video]

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota nchini Tanzania Alikiba ameachia kionjo cha wimbo wake mpya unaotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Alikiba alichapisha video fupi kwenye mitandao ya kijamii ambayo ilimuonyesha akiimba sehemu ya wimbo huo.

Soma Pia: Alikiba Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kwa Albamu Yake

Hata hivyo, hakufichua ni lini ataachia wimbo huo na kuwaacha mashabiki wake wakiwa na hamu sana. Alikiba pia alichapisha sehemu ya mistari iliyopo kwenye wimbo huo.

Kutoka kwa video fupi aliyochapisha, inaonekana kuwa wimbo hautakuwa juu ya burudani na mapenzi kama kawaida. Katika wimbo huu, Alikiba anaonekana kuwa amebadilika na kuimba kuhusu injili.Kwenye sehemu hiyo fupi aliyochapisha mitandaoni, Alikiba anatoa shukrani kwa Mungu kwa kuwa pamoja naye.

"Walitaka niwe chini ukanipandisha, mapenzi yako siwezi kufananisha bora nikushukuru... its coming get ready," taarifa ya Alikiba ilisoma.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Rudeboy Waachia Wimbo Mpya 'Salute'

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walimsihi Alikiba aachie wimbo hivi karibuni wengi wakionyesha hamu na msisimko.

Tangazo la wimbo huo kuachiliwa hivi karibuni na Alikiba linakuja muda mfupi baada yay eye kufanya kazi na mwanamuziki wa Nigeria Rude Boy kwenye wimbo wa ‘Salute’.

‘Salute’ ilipokelewa vizuri na hadi sasa ina watazamaji takriban milioni tatu kwenye YouTube.

Kabla ya hapo, Alikiba alikuwa ameachia ‘Ndombolo’ akishirikiana na wanamuziki kutoka kwa lebo ya rekodi ya King's Music. ‘Ndombolo’ pia ilifanya vizuri na kuvuma sana kwenye mtandao.

Ngoma hizi zinakisiwa kuwa miongoni mwa nyimbo zitakazokuwa kwenye albamu yake Alikiba inayotarajiwa baadae mwakani.

Tazama Video HAPA.

Leave your comment