Alikiba Awasihi Wanamuziki Kutoachia Wimbo Kwa Sababu ya Kuwania Tuzo

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Alikiba amezungumzia umuhimu wa tuzo katika taaluma ya muziki, akisema kuwa tuzo huwapa wasanii motisha, lakini si vyema kutoa muziki na nia ya kupata tuzo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Rudeboy Waachia Wimbo Mpya 'Salute'

Akizungumza na wanahabari baada ya kutua nchini Kenya, Alikiba alisema kuwa wanamuziki wanafaa kufanya kazi yao na nia ya kuwafurahisha wafuasi wao, lakini sio kutuzwa.

"Inategemea na jinsi mtu ameset mind yake, anafanya kazi yake ili aweze kupata awards ama kufanikiwa kimaisha. Kwa sababu awards sio mafanikio, before hazikuwepo lakini still watu walikua na mafanikio. Lakini hiyo hatuwezi tukaisema sana kwa sababu kila mtu anaangalia jinsi anavyopenda. Tusifanye mziki kwa sababu ya tuzo. Tufanye mziki kwa sababu ya maisha," Alikiba alinena.

Soma Pia: Alikiba Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kwa Albamu Yake

Msanii huyo ako nchini Kenya katika harakati za kurekodi collabo mpya. Katika mahojiano na Jalang’o TV, Alikiba alieza kuwa atakuwa akifanya kazi na msanii tajiki, lakini alikataa kusema jina la msanii huyo.

Alikiba amefanikiwa hivi karibuni katika nyimbo alizoachia. Katika kipindi cha mwezi mmoja, ametoa wimbo ‘Ndombolo" akishirikiana na wanamuziki kutoka lebo yake ya King's Music, kasha akaachia ‘Salute’ akishirikiana na mwanamuziki wa Nigeria Rude Boy.

Kwa sasa Alikiba amesema anashughulikia alabamu yake ambayo imekamilika asilimia 90%.

Leave your comment