Alikiba Azungumzia Mwanawe Kuingia Kwenye Muziki

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Alikiba kwa mara ya kwanza amezungumza kuhusu mtoto wake kujiunga na tasnia ya muziki. Alikiba akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, alidai kwamba amempa mtoto wake uhuru wa kuchagua tasnia yoyote ya kazi ambayo anataka.

Soma Pia: Alikiba Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kwa Albamu Yake

Mtoto wa Alikiba alipata umaarufu mitandaoni baada ya kuonekana akicheza pamoja na baba yake. Wawili hao walikuwa wakicheza wimbo wa hivi karibuni wa Alkiba uliopewa jina la 'Ndombolo'.

Video ambayo ilimshirikisha mtoto wa Alikiba ilienea sana kwenye mtandao na mashabiki wengi waliipenda. Hii ilileta udadisi na maswali ikiwa Alikiba alikuwa akimuandaa mtoto wake kwa kuingia kwenye tasnia ya muziki.

Soma Pia:Alikiba, Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour ‘Ndombolo’: Nyimbo Mpya Tanzania 

Kulingana na Alikiba, hatamlazimisha mtoto wake kujiunga na tasnia ya burudani. Hata hivyo alisema kuwa muziki unaendeshwa katika familia yake, na kuongeza kuwa mtoto wake anapenda muziki.

"Singependa kumhusisha kwenye mambo yangu bana, hadi atakapochagua kazi yake yeye. Anapenda muziki sana, muziki upo kwenye damu. Unajua pia naye anapenda muziki, baba yake pia ni mtu wa muziki sana. Unajua vitu vinavyopendeza zaidi ata familia wakiona wana support," Alikiba alisema.

Alikiba ni mmoja wa wanamuziki wakubwa nchini Tanzania. Kiba amekuwa kwenye tasnia ya muziki na ni miongoni mwa wasanii wakongwe ambao bado wanafanya vizuri sana.

Leave your comment