Ommy Dimpoz Atia Kando Ugomvi wake na Diamond

[Picha: Ommy Dimpoz | Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ommy Dimpoz ametangaza kuwa ameweka kando tofauti zake za kimuziki na mwenzake Diamond Platnumz.

Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz wamejulikana kuwa wapinzani kwa muda mrefu sana. Miaka michache iliyopita, wawili hao walihusika kwenye mabishano kwenye mitandao ya kijamii. Walibadilishana na kurushiana maneno machungu na tangu wakati huo, hawajawahi kuwa na uhusiano mzuri tena.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Wimbo Mpya ‘Sandakalawe’

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni na Wasafi TV, Muimbaji huyo alisema kuwa hajivunii vitu kadhaa alivyofanya hapo awali ikiwa ikiwemo kumshirikisha Mama Dangote kwenye malumbano yake na Diamond.

"Kiukweli kwa upande wangu, unajua unapokuwa kijana kwenye mambo ya ubishani kwenye mitandao knakuwa na mihemko... Wakati mwingine unaweza kufanya kitu baada ya ukaona kuwa hizi hakikuwa sawa ... kwa kweli naezasema kukosea kwa upande wangu kwakumhusisha bi kubwa ambaye naheshimiana naye…,” alisema Dimpoz.

Soma Pia: Jay Melody Kuachia Remix ya ‘Najieka’ Akimshirikisha Shilole

"Mimi nafsi yangu, kwanza nitakuambia ukweli nimetoka kufanya ibada nimemwomba Mungu anisamehe na watu ambao niliwakosea pia waweze kunisamehe. Kwa hiyo sina kinyongo na mtu, sina shida na mtu, siitaji tatizo na mtu," Ommy Dimpoz aliongezea.

Kwenye mahojiano hayo, Ommy Dimpoz pia alkanusha madai kuwa ana uhasama na Alikibiba. Kulingana na Dimpoz, Alikiba ni rafiki yake wa karibu na wako kwenye hali nzuri, ijapokuwa hawakutani na kuonekana pamoja mara kwa mara kama kitambo.

Leave your comment