Jay Melody Kuachia Remix ya ‘Najieka’ Akimshirikisha Shilole

[Picha: Jay Melody Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka 2021 ni mwaka wa Jay Melody. Miezi mitano iliyopita, amewaachia ngoma mbili matata ‘Huba Hulu’ na ‘Najieka’ akishirikiana na mtayarishaji wa muziki JiniX66.

Akiongea kwenye kipindi cha burudani cha XXL, Jay Melody ametangaza ujio wa remix ya wimbo wa Najieka akishirikiana na msanii Zuena Mohamed almaarufu kama Shilole.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo Mpya ‘Kamata’

"Hii ni exclusive kabisa, ‘Najieka’ inaweza ikatoka soon remix yake ambayo nimeimba na msanii mkubwa wa kike na ofcourse ni Shishi baby. Kwa hiyo watu wakae tayari kupata remix ya Najieka," alinena Jay Melody.

Kulingana na Jay Melody, wimbo wa ‘Najieka’ umechukua ladha kutoka kwa wimbo wa zamani wa msanii Abdul Sykes almaarufu kama Dully Sykes wimbo uitwao Julietta.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Rudeboy Waachia Wimbo Mpya 'Salute'

Akiongea kwenye kipindi cha Zege Jay siku chache zilizopita Melody alinena "Siku hiyo nilichukua beat (kutoka kwa JiniX66) nikarudi nayo nyumbani lakini sikutaka kuiandikia siku hiyo hiyo, nilitaka nipoe kwanza, nikawa nasikiliza tu nyimbo nyingine ambazo watu washazifanyaga"

Jay melody aliongeza kuwa baada ya kusikiliza sana nyimbo za zamani alivutiwa na wimbo wa Dully Sykes Julietta na hapo ndipo akaanza kuandika wimbo wa ‘Najieka’.

Ukiachana na kuimba, Jay Melody pia ana karama ya uandishi ambapo mpaka sasa ameshaandika nyimbo nyingi kama ‘Do Me’ ya mwana dada Nandy pamoja na ‘Hauzimi’ ya mwanamuziki wa THT Benson.

Leave your comment