Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Wimbo Mpya ‘Sandakalawe’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi na msanii kutokea label ya Konde Music Worldwide Harmonize ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Sandakalawe’.

Soma Pia: Harmonize Atambulisha Mtandao Mpya Ataokuwa Akitumia Kutiririsha Kazi Yake Hewani

‘Sandakalawe’ umetayarishwa na Daxo Chali ambaye ni mojawapo kati ya watayarishaji muziki wakubwa hapa nchini Tanzania.

Wimbo huu sio mpya sana kwa wafuatiliaji wa muziki kwani miezi michache iliyopita Harmonize alipokuwa anamtambulisha Anjella kama msanii rasmi wa Konde Gang, aliiimba kipande cha wimbo huo ili kuburudisha mashabiki lakini hakuweka wazi atautoa lini wimbo huo ambao mpaka sasa umetazamwa takriban mara 104,000 kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]

‘Sandakalawe’ ni wimbo wa Amapiano. Kwenye verse ya kwanza Harmonize anaghani "Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa, Saidi kichwa nitamuweka wapi na mkongo nishampakaza."

Kwenye wimbo huu msanii Harmonize ametumia tamathali za semi nyingi haswa tafsida ili kupunguza ukali wa maneno. Kwenye kiitikio Harmonize anaturudisha utotoni kwa kuimba "Sandakalawe Amina aaah mwenye kupata apate Je mwenye kukosa akosee, eeeh kuku gani mweupe."

Sandakalawe umeweza kufanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube kwa sababu ndani ya dakika 30 tu ulikuwa umeangaliwa takriban mara 51,000. Kando na Sandakalawe, Diamond Platnumz pia siku ya leo aliweza kuachia wimbo majira ya asubuhi uitwao ‘Kamata’ ambao ndani ya dakika 30 ulitazamwa takriban mara 31,000.

Hii inaonesha ni jinsi gani wasanii watanzania wanafuatiliwa sana na mashabiki zao kwenye upande wa YouTube.

Bado haijawekwa wazi kama wimbo huu wa Sandakalawe utakuwepo pia kwenye albamu inayofuatia ya Harmonize, lakini mpaka sasa wimbo huu ni wimbo wa tatu wa harmonize tangu mwezi Juni uanze, nyingine zikiwa ni ‘Tuvushe’ pamoja na ‘Kazi iendelee’ zilizotoka Juni 12 mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=ISEQ6fldt5Y

Leave your comment