Meja Kunta Awasihi Wasanii wa Tanzania Hasa wa Singeli Kutumia Kiswahili

[Picha: Meja Kunta Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Meja Kunta ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake uitwao ‘Kidimbwi’ ametoa rai kwa wasanii wenzake hasa wa muziki wa Singeli kutumia lugha ya kiswahili pale ambapo wanatunga nyimbo zao.

Kunta ameyasema hayo wakati anafanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini Tanzania ambapo Kunta alikaririwa akisema "Ningepeenda tuimbe Kiswahili maana hata hao wenzetu wanaimba lugha zao, ukiimba kiingereza unaua lugha yako."

Soma Pia: Muziki wa Singeli Tanzania: Kwa Nini Singeli Haitambi Kama Bongo Fleva?

Kauli hiyo inakuja wiki kadhaa tangu msanii mwenzake wa Singeli Mc Kinata kutoa wimbo wa singeli kwa lugha ya kiingereza uitwao Do Let Mi Go aliomshirikisha msanii Ibraah kutokea Konde Gang.

Wimbo huo umependwa sana na mashabiki na mpaka sasa umetazamwa takriban mara Milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Meja Kunta Aachia Video Mpya ‘Madanga ya Mke Wangu’Akimshirikisha D Voice

Aghalabu muziki wa Singeli huonekana kama ni muziki wa mtaani na uswahilini hivyo Mc Kinata kuimba singeli kwa lugha ya kiingereza kilionekana ni kitu kipya na cha utofauti sana.

Meja Kunta aliongeza kwa kusema "Inawezekana nyimbo kuhit hata kwa lugha ya kiswahili wenzetu hawaimbi lugha yetu." Meja Kunta kwa muda mrefu sasa ameweza kutengeneza nyimbo nzuri ambazo zimegonga mioyo ya mashabiki kama vile "madanga ya mke wangu" ambao umetazamwa mara milioni na laki tatu huko YouTube, "Sina" aliomshirikisha malkia Karen, "Mamu" pamoja na "wanga wabaya" aliomshirikisha Lavalava msanii kutokea WCB wimbo ambao pia ulipendwa na mtayarishaji muziki kutokea nchini marekani Swizz Beats.

Kando na hilo, kwenye mahojiano hayo Meja Kunta ameweka wazi kuwa ameshafanya nyimbo na wasanii kadhaa wa Tanzania kama vile Young Lunya, Marioo, Nandy, Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz.

Leave your comment