Nyimbo Mpya: Meja Kunta Aachia Video Mpya ‘Madanga ya Mke Wangu’Akimshirikisha D Voice

[Picha: Meja Kunta Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa muziki aina Singeli Meja Kunta ameachia video yake mpya kwa jina.

Kwenye wimbo huu, wanaimba kuhusu uzuri wa udangaji wa mwanamke

“We jamani mke wangu anadanga lake, mwenzenu ananikosha, We kila siku ikifika morning Lazima atume pesa…” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Albamu yake Mpya ‘Definition of Love’

Kwa kifupi wawili hao wanaangazia hadithi ya mwanamume mmoja ambaye amefanya madanga ya mke wake kuwa biashara ya kujikimu.

‘Madanga ya Mke Wangu’ ni kazi ya pili mwaka huu kutoka kwa Meja Kunta. D Voice kwa upande wake amedhihirisha ubabe wake katika muziki wa Singeli haswa anapoanza wimbo huu.

Waigizaji kwenye wimbo huu ni Dulvani na Aladin Mendrad huku waelekezaji wa kanda hii wakiwa Creator Pro 5 na Mwaiba wa Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa Youtube huku nambari za watazamaji zikiwa elfu arobaini na tano.

Meja Kunta ni mojawapo ya wasanii nguli wa muziki wa Singeli ambao kufikia sasa wanendelea kujitafutia hadhi katika fani nzima ya mziki wa Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=NaPt97DwWzY&ab_channel=MejaKunta

Leave your comment