Nikki wa Pili Kubaki na Kikundi cha Weusi Licha ya Kuapishwa Mkuu wa Wilaya
23 June 2021
[Picha: Weusi Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Msanii wa Hip-hop kutoka Tanzania Nikki Wa Pili ambaye pia ni mwanachama wa Kundi La Weusi amezungumza kuhusu mkondo ambao atauchukua kama mwanamuziki baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Weusi Waachia Albamu yao Mpya 'Air Weusi'
Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kwake, Nikki alisisitiza kuwa bado alikuwa mshiriki wa Kundi La Weusi licha ya uteuzi huo. Nikki, hata hivyo, alifafanua kwamba atachukua majukumu mengine katika bendi na sio lazima aendelee kuimba kama hapo awali.
Alielezea kwamba sio lazima awe kwenye jukwaa ili aonekane kama mshiriki wa kikundi hicho. Kulingana na Nikki, bado atachangia maoni ambayo yatakayosaidia Kundi La Weusi katika kufanya uamuzi mbali mbali za kimziki.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Weusi Wamshirikisha Khadija Kopa Kwa Wimbo Wao Mpya ‘Penzi la Bando’
Aidha, msanii huyo anaamini kuwa kuna njia nyingi ambazo angeweza kushiriki katika bendi la Kundi La Weusi na bado kuwa mkuu wa Kisarawe kwa wakati mmoja.
"Si lazima labda niwepo kwenye ziara, lakini naweza kutoa ushauri, na maoni yako kwenye mpango. Kwa hivyo sanaa ni uwanja wa uwanja unaoweza kuwa na uwezo wa kutofautisha sana. Kwa hiyo mchango wangu kwa weusi utaendelea kuwepo," Nikki alinukuliwa na gazeti la The Citizen.
Nikki aliendelea kwa kufafanua kuwa bado atashiriki katika tasnia ya burudani ya Tanzania na ataendelea kuwahudumia mashabiki wake japo katika nafasi tofauti. Wanachama wengine wa Kundi La Weusi pia walijitokeza kumuunga mkono Nikki Wa Pili wakati wa kuapishwa kwake.
Leave your comment