Nyimbo Mpya: Weusi Waachia Albamu yao Mpya 'Air Weusi'

[Picha: Weusi Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kundi la wanamziki wa Hiphop kutoka Tanzania Weusi wameachia rasmi album yao mpya kwa jina 'Air Weusi'.

Weusi ni kundi la wasanii wanne almaarufu; Gnako Warawara, Nikki Wa Pili Joh Makini na Lorde Mweusi ambao wamekua kwenye fani ya mziki kwa muda mrefu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Weusi Wamshirikisha Khadija Kopa Kwa Wimbo Wao Mpya ‘Penzi la Bando’

‘Air Weusi’ ni albamu yenye nyimbo kumi na nne na mbili tu ndio za ushirikiano. Walioshirikishwa kwenye albamu hii ni pamoja na Bi. Khadija Kopa na Big Boss J.O.J.O.

Katika makundi yote ya hip hop Tanzania, Weusi wameendelea kufanya mziki wao bila kujali yanayosemwa kuhusu mziki wa hip hop nchini humo.

Hivi karibuni waliachia kanda ya wimbo wao ‘Penzi la Bando’ ambapo Khadija Kopa kwa mara nyingine alidhihirisha ubabe wake katika sanaa ya mziki.

‘Penzi la Bando’ ni wimbo unaoangazia mambo yanayotondeka katika jamii haswa uhusiano kati ya binadamu na mitandao yao.

Waandaji wa albamu hii ni kama vile S2kizzy, Luffa, Davy Machords, Drama boy, Nahreel na Goncher Beats.

Albamu hiyo sasa inapatikana katika mitandao yote ya mziki. Hii hapa orodha ya nyimbo kwenye album hio:

 1. Intro
 2. Air Weusi
 3. Ile sasa
 4. Derby
 5. Iko Mambo
 6. Interlude
 7. Manje
 8. Mbuppu
 9. Summertime ft Big Boss Jojo
 10. Tout Le Monde
 11. Videadly
 12. Kamata toto
 13. Machete
 14. Penzi La Bando ft Bi. Khadija Kopa

https://www.youtube.com/watch?v=vnIeXFqYjmA

Leave your comment