Nyimbo Mpya: Weusi Wamshirikisha Khadija Kopa Kwa Wimbo Wao Mpya ‘Penzi la Bando’

[Picha: Weusi Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Bendi maarafu kutoka Tanzania Weusi wameanza safari yao ya muziki mwaka huu na wimbo mpya uitwao ‘Penzi La Bando’.

Katika ‘Penzi La Bando’ wamemshirikisha Malkia wa michambo Bi. Khadija Kopa ambaye ameutendea haki wimbo huu.

Soma Pia: Nyimbo Tano za Rayvanny Zilizompa Umaarufu Bongo

Wimbo huu unaangazia mambo yanaotondeka katika jamii haswa uhusiano kati ya binadamu na mitandao yao.

 “,,,Nikikata wanapanda wengine hewani (bando), una data na huna mtandao mwingine(Bando),Kama humtii wanamtia wengine(Bando),unatumia mtandao mmoja wanatumia miwili,(Bando),mwnaume akidata na kifurushi(Bando),mtoto ndio anapata kifurushi,,,” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huo.

Wimbo huu umetayarishwa na S2Kizzy huu ukichanganywa na kubuniwa na Chizan Brain.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Kiuno’

Khadija Kopa kwa upande wake alidhihirisha ubabe wake kwa sauti nzuri kwenye wimbo huu.

Kufikia sasa Weusi wameachia audio tu huku kanda ya wimbo huu ikitarajiwa hivi karibuni.

Kupitia mtandao wao wa Instagram, Bendi ya Weusi imetangaza ujio wa kanda ya wimbo huu wakati wowote sasa.

“Tulipanga kuachia movie yetu ya PENZI LA BANDO leo lakini kutokana na maombolezo yanayoendelea tunaomba MOVIE iendelee siku ya Jumatatu”.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya elfu thelathini na mbili.

 https://www.youtube.com/watch?v=ox8H45JFX7o&ab_channel=WEUSI

Leave your comment