Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Kiuno’

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Yako Kwenye WhatsApp

Msanii kutoka lebo ya Wasafi Rayvanny ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Kiuno’.

‘Kiuno’ ni mojawapo ya nyimbo 23 kwenu albamu yake ya ‘Sound from Africa’.

‘Kiuno’ Ni wimbo unaoangazia namna Rayvanny anavyopagawishwa na kiuno cha mpenzi wake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Album 4 Zinazofanya Vizuri Bongo Mwaka wa 2021

"Baby baby... Michepuko ya Zamani bye bye, MI najidai dai dai, ooh we subiri shera.... Zungusha pepeta ungo,nipe mambo yakizania mafumbo, Geuza onyesha umbo, jiachie wala usibane tumbo..." hii Ni baadhi ya mistari kwenye wimbo huu.

Kanda hii inamvutio mkubwa kwani mavazi yaliyotumika ni yale yanaonyesha uhalisia wa kiafrika.

Mabinti waliomo pia hawakuzembea katika kusakata densi ya ‘Kiuno’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

Kwingineko Ni kuwa mdundo wa wimbo huu ni kama ule wa mziki wa Rhumba kutoka Congo.

Kwa kadri yake, Rayvanny ameufanyia wimbo huu kazi nzuri sana.

Unapoitazama kanda hii, unaona ujuzi mkubwa kutoka Kwa Director Kenny wa Zoom Extra ya WCB.

Video ya wimbo hii imepokelewa vizuri kwenye YouTube huku nambari za watazamaji zikiongezeka kwa kasi muda unapozidi kusonga. Hii ni dhihirisho ya ubabe wa fundi huyu wa mziki Rayvanny.

Kufikia sasa, albamu yake Rayvanny ‘Sound from Africa’ imepata usikilizaji mkubwa sana kote ulimwenguni. Albamu hio imesikizwa na mamiliona ya watu, nan i moajwapo ya kazi za kimuziki zinazofanya vyema Afrika nzima mwezi huu wa Februari.

https://www.youtube.com/watch?v=r573wpRMtaA

Leave your comment

Top stories

More News