Nyimbo Mpya: Album 4 Zinazofanya Vizuri Bongo Mwaka wa 2021

[Photo Credit: Rayvanny Instagram]

By Branice Nafula

Share on WhatsApp

Mwaka huu wa 2021 ulianza na mashamra huku wasanii kadhaa kutoka Bongo wakiachia album zao.

Katika nakala hii, tunaangazia album zinazofanya vizuri nchini Tanzania mwezi huu wa Februari 2021.

Slave Becomes a King - Darassa

Album hii ilachiliwa mwaka ukianza na ina nyimbo 21. Katika album hii, Darassa amewashirikisha wasanii tajika Africa kama vile; Alikiba, Femi One na wengine wengi.

'Slave Becomes a King' imepokelewa vyema na ni miongoni mwa album zilizotiririshwa sana mtandaoni mwaka huu.

Sound from Africa - Rayvanny

Hii ndio album ya kwanza yake Rayvanny tangu aanze kufanya mziki. Aliiachia tarehe moja February na kufikia sasa, ni moja wapo ya album inayosikizwa  kote ulimwenguni.

Wimbo wa 'Lala' kwenye album hio  imezua gumzo mtandaoni kwa sababu ya maudhui yake. ‘Sound From Africa’ ni album ya kipeee inayohusisha mziki wenye asili ya kiafrika tu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

Burudani EP - Chege Chigunda

Chege Chigunda alitoa EP hii wiki kadhaa zilizopita. Kulingana na Chege, baada ya kuwa na album kadhaa katika sanaa ya mziki, aliona akaachie EP kama zawadi kwa mashabiki wake. EP ya Burudani ina nyimbo 6. Kwa sasa Chege ameachilia video moja (Burudani) kwenye EP hio.

Soma Pia: Rayvanny’s ‘Sound From Africa’ Album Debuts on American Billboard

Refreshmind - Barnaba

Album hii ina nyimbo kumi na nne. Kwenye album hii, Barnaba amewashirikisha  wasanii mbali mbali, wengi wakiwa wa Tanzania.

Hivi maajuzi, Barnaba aliachilia video ya wimbo ‘Kizungumkuti’. 

Leave your comment