Mama Dangote Awaelimisha Watanzania Jinsi ya Kumpigia Kura Diamond Kwenye Tuzo za BET

[Picha: Routine Blast]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mama Dangote; mamake mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz amejitokeza kuwaelimisha watumiaji wa mitandao ya kijamii jinsi wanaweza kumpigia kura mwanamuziki huyo kwenye Tuzo za BET.

Diamond aliteuliwa kwenye tuzo za kifahari katika kitengo cha Best International Act. Bosi wa WCB atashindana na wanamuziki wengine wakuu wa Afrika wakiwemo Burna Boy na Wizkid.

Soma Pia: Diamond Platnumz Ateuliwa kwa Tuzo za BET 2021

Mama Dangote alielezea kwenye chapisho la mitandao ya kijamii kwamba wanaotaka kumpigia kura Diamond wanapaswa kutembelea kurasa za mtandao za kijamii za BET na kutoa maoni yao kwa maneno "I Vote For Diamond Platnumz".

"Ili Kumuwezesha Diamond Platnumz Kushinda Tuzo Za @betawards Kwenye Kipengele Cha Best International Act unatakiwa kwenye kila post yako unayompost Diamond Platnumz Kwenye Social media zako (Instagram, Twitter, Facebook n.k) Iwe Picha Au Video Yeyote Ya Diamond Platnumz unatakiwa uambatanishe na maneno (Caption) Hiyo Apo "I Vote For Diamond Platnum," chapisho la mitandao ya kijamii lilisoma. "Pia unaweza Kwenda Ku comment kwenye page za Tuzo Husika Maneno Hayo Hayo bila kukosea," taarifa iliendelea.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Zuchu, Rayvanny, Mbosso na Lava Lava Mwezi Mei 2021 [Video]

Watanzania wamejitokeza kwa wingi kumfanyia kampeni Diamond Platnumz. Watu mashuhuri wameelezea kumuunga mkono Diamond Platnumz huku wakiwasihi watanzania wampigie kura Diamond.

Leave your comment