Diamond Platnumz Ateuliwa kwa Tuzo za BET 2021

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania tuzo ya BET mwaku huu wa 2021.

Hii ni baada ya BET kuweka wazi orodha kamili ya watakaowania tuzo mbali mbali mwezi Juni tarehe 27.

Soma Pia: Tamasha la Siku ya Afrika: Zuchu Atumbuiza Mashabiki na Ngoma Zake Sukari, Cheche [Video]

Diamond Platnumz ameteuliwa kwenye kipengele cha Best International act na anahitaji kura za mashabiki wake ili kushinda tuzo hilo.

Kulingana na orodha iliyotolewa, Diamond Platnumz ndio msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.

Orodha hio pia ina wasanii tajika kama vile Wizkid na Burna Boy wa Nigeria, Emicida wa Brazil, Headie wa Uingereza, Aya Nakamura na Youssoupha wa Ufaransa na Young T na  Bugsey wa Uingereza.

Soma Pia: Rayvanny Atajwa Msanii wa Pili Bongo Mwenye Mauzo Makubwa ya Muziki

Katika shughuli hii nzima, BET inatambua wasanii, watumbuizaji, na wanariadha.

Oradha hii ilioachiwa leo ilipitishwa na chuo cha upigaji kura wa BET ambao wahusika wakuu ni mashabiki na kikundi kinachoheshimika cha wataalamu wa burudani katika uwanja wa televisheni, filamu, muziki, mitandao ya kijamii, uuzaji wa kidijitali, uandishi wa habari za michezo, uhusiano wa umma, na sanaa ya ubunifu.

Nchini Tanzania, Rayvanny pekee ndio msani ambaye ashawai kushinda tuzo la BET.

Kwenye eneo la Afrika Mashariki, tuzo hilo limeshindwa na Rayvanny na Eddy Kenzo kutoka Uganda.

Mwaka uliopita, msanii wa Kenya Khaligraph Jones aliteuliwa kwa tuzo za BET lakini hakufanikiwa kushinda.

Leave your comment