Rayvanny Atajwa Msanii wa Pili Bongo Mwenye Mauzo Makubwa ya Muziki

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkuu wa Dijitali kwenye lebo ya WCB Wasafi Kim Kayndo amesema kuwa ukimuondoa Diamond Platnumz, Rayvanny ndiye msanii anayeongoza kwa mauzo makubwa kwenye mtandao ya dijitali.

Kim akizungumza katika mahojiano, alisema kuwa Rayvanny anapata pesa mingi kupitia mitandao hiyo ya mziki na ndani ya Afrika Mashariki nzima hakuna msanii yeyote anayemfikia kwa sasa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya ‘Kiss Me’

“Ukimtoa Diamond, Rayvanny ni mtu amabaye anainguiza hela nyingi kwenye Digital Platforms nchini East Africa. Yaani hilo halina mjadala ndio iko na facts zipo,” alisema Kim.

Mwezi Februari mwaka huu, Rayvanny aliachia albamu yake ‘Sound from Africa’ yenye nyimbo ishirini na tatu.

Kufikia, sasa ni mojawapo ya kazi iliochezwa zaidi kwenyemitandao ya kidijitali. Inakisiwa kuwa albamu hio imetiririshwa na zaidi ya watu milioni mia moja ishirini.

Wakati wasanii na mashabiki wanaendelea kubishana kuhusu uhalisia wa nambari za watazamaji kwenye mitandao hii, Rayvananny anaingia kwenye orodha ya wasanii wanaopata kipato kizuri kwa kazi yao ya mziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Kwa sasa, Rayvanny ameachia videonne kutoka kwenye albamu ya ‘Sound from Afrika’. Kanda hizi ni kama vile; Kiuno, Lala, Number One Remix na Kelebe.

‘Kelebe’ inaendela kupata umaarufu zaidi kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya milioni moja.

Leave your comment