Tamasha la Siku ya Afrika: Zuchu Atumbuiza Mashabiki na Ngoma Zake Sukari, Cheche [Video]

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota ya msanii Zuchu inaendelea kung’aa baada ya yeye kupata fursa ya kuwatumbuiza mashabiki kwenye hafla ya ‘Siku ya Afrika’ iliyoandaliwa Mei 25. 2021.

Kwenye tamasha hio, Zuchu aliwatumbuiza mashabiki na nyimbo zake ‘Cheche’ na ‘Sukari’. Zuchu alinza na wimbo wake wa ‘Cheche’ alioimba kwa ustadi mkubwa na kisha akamaliza na ‘Sukari’.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Safari yake ya Usanii na Kuachia Ngoma Zinazovuma Zanzibar na Dar es Salaam

Tofauti na mwaka uliopita ambapo Diamond Platnumz aliweza kufanya show yake kutoka nyumbani kwake, Zuchu alisafiri hadi Afrika kusini akiwa na mtayarishaji wa densi wa Wasafi Angel Nyigu kuandaa kazi ya show hiyo.

Mwaka huu, dhamira ya tamasha hii ni kuungana pamoja dhidi ya Ugonjwa wa Malaria.

Tamasha hilo limewaleta pamoja wasanii na waigizaji wengi haswa wenye asili ya Afrika ili kusaidia katika shughuli nzima.

Soma Pia: Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Wasani wengeni tajika walioweza kuhudhuria ana kuwatumbuiza mashabiki kwenye hafla hii ni kama vile; Bahati (Kenya),Bella Shmurda (Nigeria),Blaq Diamond (South Africa),Elaine (South Africa),Focalistic (South Africa), Gyakie (Ghana), Omah Lay (Nigeria), Suspect 95 (Ivory Coast),Teni (Nigeria), Rozzy Sokota (Sierra Leone),Ary (Angola),Mohamed Ramadan (Egypt), Nadia Mukami Kenya na wengineo.

Shughuli nzima ya siku ya Afrika iliendeshwa na Muigizaji wa filamu Idris Elba kwenye jukwa la MTV Base.

https://www.youtube.com/watch?v=_NahNbAkCDc&ab_channel=Zuchu

Leave your comment