Zuchu Azungumzia Safari yake ya Usanii na Kuachia Ngoma Zinazovuma Zanzibar na Dar es Salaam

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa mziki wa Bongo Zuchu ni moja kati ya wasanii wachache nchini Tanzania waliopata umaarufu kwa muda mfupi sana.

Akizungumza katika mahojiano, Zuchu alisema kuwa akiwa msanii mchanga,  ndoto yake ilikuwa kufanya mziki itakayovuma Zanzibar and Dar es Salaam.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Kwa sasa ana furaha kuwa mziki wake umepokelewa vizuri cnhni Tanzania na hata barani Afrika.

“Nakumbuka nilivyokua mdogo wasanii wa kizanzibari walikua wanajaribu sana kufanya mziki mzuri, ukiwa huko nyimbo inahit lakini ukiingia Dar es Salaam watu wachache sana wanaijua na mpaka uwaambie waitafute, Kwa hiyo moja ya ndoto zangu , nilikua nasema siku moja ntakuja kufanya mziki na nisigawanyishwe, nikienda Zanzibar nikute mziki wangu na nikiwa Dar niupate, bara Afrika yaani kote, kwa hiyo sasa naishi kwenye ndoto zangu….” alisema Zuchu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya ‘Kiss Me’

Wakati anatarajiwa kutumbuiza katika sherehe za Mwenge wa Uhuru huko Zanzibar, Zuchu alishukuru Serikali wanavyompokea na hata kumpa fursa ya kuendelea na kazi yake ya utumbuzaji.

“…Na nafurahi sana kwa sapoti nilinayo kutoka Zanzibar kwa kiwango hiki, unajua sapoti ya ulikotoka ni muhimu mno, nashukuru serikali inasapoti vile inavyotakikana…." alisema Zuchu.

Vile vile ameahidi kupiga show lenye ladha ya taarab akitaja kuwa yeye ni taarab tosha. Ikumbikwe kwamba , ndani ya mwaka mmoja Zuchu amepata umaarufu kupitia mziki wake ndani ya lebo ya wasafi.

Leave your comment