Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Zuchu, Rayvanny, Mbosso na Lava Lava Mwezi Mei 2021 [Video]
1 June 2021
[Picha: Rayvanny Instagram]
Mwandishi: Omondi Otieno
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Kelebe - Rayvanny ft Innoss’B
Huu ndio wimbo ulioachiwa na Rayvanny akimshirikisha msanii gwiji kutoka Congo Innoss’B. Mwezi Mei ‘Kelebe’ ilichukua nafasi ya kwanza kwenye trends na watazamaji zaidi ya milioni tatu nukta mbili kwenye mtandao wa YouTube.
Soma Pia: Diamond Platnumz Ateuliwa kwa Tuzo za BET 2021
Yes - Mbosso ft Spice Diana
Huu ni wimbo wa kumuomba mchumba kuwa mke wa mtu au tuseme harusi. Kwenye huu, wimbo Mbosso alimshirikisha Spice Diana kutoka Uganda. ‘Yes’ ni mojawapo ya ngoma kwenye ‘Definiion of Love’ album alioachia Mbosso.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]
Komesha – Lava lava
‘Komesha’ ni wimbo mpya kutoka kwa msanii Lava Lava. Katika ngoma hii, Lava Lava anapigania penzi lake. Kufikia sasa, ‘Komesha’ ina watazamaji zaidi ya milioni moja.
Sere- Olakira ft Zuchu
Kwenye wimbo huu, msanii wa Nigeria Olakira amemshirikisha Zuchu. Hii majowapo ya ngoma kutoka kwenye ‘4Play’ EP yake Olakira. Kwa sasa ngoma hii ina watazamaji zaki ya milioni moja nukta tisa kwenye YouTube.
Kazi Iendele – Zuchu na Rayvanny
Zuchu na Rayvanny waliachia nyimbo mbili tofauti zenye mada sawa ‘Kazi Iendelee’.
Wawili hawa waliachia kazi hii kumsifia rais wa Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu.
Katika wimbo wa Zuchu, anahadithia historia ya Rais Suluhu katika siasa kuanzia alipokuwa makamu wa Rais chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa Tanzania marehemu Dkt. John Pombe Magufuli alieaga mwezi mmoja uliopita.
Kwa upande wake Rayvanny alimsifia Rais Samia kama mama wa taifa na kama wananchi wanampa pongezi kwa kuhimiza kuwa 'Kazi iendelee'.
Katika mistari yake, anaanza kwa kukumbuku za kifo cha marehemu rais Magufuli jinsi wanachi walivyohuzunika na kuvunjika mioyo kuhusu kifo cha rais huyo.
Rayvanny anaimba kuwa 'Kazi iendelee' katika sekta mbali mbali kwani aliye kwenye usukani anajali maslahi ya wananchi wake.
Leave your comment