Nyimbo Mpya: Jux, Jay Rox na Kenz Ville Waungana Kuachia Wimbo Mpya ‘Changanya’

[Picha: Juma Jux Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Bongo Juma Jux ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Changanya’. Katika wimbo huu, Jux amefanya kushirikishwa na wasanii wa Zambia Jay Rox na Kenz Ville Marley.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jux Adondosha Kanda ya Wimbo Mpya ‘Bado Yupo’

Wimbo huu ni wenye maudhui ya kujiburudisha na kufurahia huku waimbaji hao wakiwasifia kina dada kwa kucheza kwao.

Jay Rox anaanzisha wimbo huu kwa lugha ya Nyanja kutoka Zambia akisifia jinsi anavyopagawishwa na minenguo yake.

“Ama oneka so simple, Niotelela no pimple, Baka toloma ba people,Aka pita bamaliza pinto,Akayamba kuvi changa, changa changa, changa,Changa kuvi changanya O Kuvi changa, change…” aliimba Jay Rox.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Jux Zinazovuma 2021

Kisha Jux anaingia kwa Lugha ya Kiswahili pia akisifia umbo la dada mmoja huku akisema vile anamchanganya kwa sana.

Jux anaimba jinsi dada yule amemteka na hata kumalizia hela zake za akiba. Kenz Ville Marley pia hakuachwa nyuma alipoingiza sauti yake kwenye kazi hii kwa ujuzi mkubwa.

Hivyo, wimbo huu ni wa kusifia uzuri wa kina dada wa Kiafrika. Ushirikiano huu ni mzuri kwa wasanii hawa wa Zambia wakati wanamziki wa bara la Afrika wanajaribu kuunganisha sauti ya mziki wa Kiafrika bila changamoto za lugha. Kwa sasa wimbo huu unaendelea kupokelewa vizuri kanda yake ikitarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=c-7IrZVVnD8

Leave your comment