Nyimbo Mpya: ‘Kelebe’ ya Rayvanny, Innoss’B na Ngoma Tano Zilizoachiwa Bongo Wiki

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ndani ya wikendi iliyopita wasanii wa mziki wa Bongo hawakulegea kwa kuachia kazi mpya. Katika nakala hii, tunaangazia Nyimbo mpya zilizoachiwa Bongo wikendi iliyopita:

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

Kelebe ‐ Rayvanny ft Innoss’B

Huu ni wimbo ambao Rayvanny aliachia siku ya Ijumaa. ‘Kelebe’ ni moja ya nyimbo zilizoko kwenye albamu mpya ya Rayvanny ‘Sound From Africa’. ‘Kelebe’ ni mziki wa kusisimua hisia za usakataji na umepokelewa kwa kishIndo. Kwa sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni moja nukta nne.

https://www.youtube.com/watch?v=V7sBxHz_nHE

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Nobody ‐ Anjella

Huu ni wimbo wa pili wa msanii Anjella tangu kuzinduliwa rasmi na label ya Konde Music Worldwide. Katika Nobody, Anjella anaeleza kuwa hamna atakaempenda mpenzi wake kumshinda yeye. Kwa sasa, wimbo huu una watazamaji zaidi ya milioni moja nukta tisa ndani ya wiki moja.

https://www.youtube.com/watch?v=-NCqC_BoUXc

Komesha ‐ Lava lava

Huu ni wimbo ambao Lava lava anasifia urembo wa mwanadada mmoja ambae anampendeza yeye. Kufiki sasa ni wimbo ulio na watazamaji laki saba.

https://www.youtube.com/watch?v=XmT_CsFAtqc

I Do ‐ Wini ft Darassa

Huu ni wimbo wa mapenzi ambao Wini amemshirikisha gwiji wa rap Darassa. Katika wimbo huu, wawili hao wanamwagiana sifa jinsi wanavyopendana. Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=BIrzMEsHll0

999 ‐ Nikki Mbishi

Kwenye ngoma hii, Nikki anajipigia upatu kama king wa rap. Vile vile anawachana wasanii wakubwa wanaondelea kudhalilisha wasanii wengine. Anaonya kuwa tabia hizo zinakandamiza sanaa.

https://www.youtube.com/watch?v=BtCGQ3r45qk

Leave your comment