Anjella Aachia Wimbo Mpya wa Mapenzi Kwa Jina ‘Nobody’

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi kutoka lebo ya Konde Music Worldwide Anjella ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Nobody’.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Huu ni wimbo wa mapenzi ambapo Anjella anasifia uzuri wa mapenzi. Katika ‘Nobody’, Anjella anatuambia kuwa hakuna mtu atakayempenda mpenzi wake kama yeye na hakuna mtu atakayeingilia mapenzi yao na yuko tayari kumpeleka mpenzi wake kwa mama yake ili amuone.

Soma Pia: Konde Music Worldwide Kuachia Albamu Nne Mwaka wa 2021

Anaanza kwa kusifia jinsi mpenzi wake humkosha na kusema kuwa yeye ni Pacha wake.

“Na vile unanikoshaga nadata mwenzako, The way you love me love me nakonda mwenzako (Mmmh) Aaah!,Na tumeumbwa wawili wili,Na wewe ndo moja mimi mbili mbili,Usije niwashaga pilipili mimi pacha wako…” aliimba Anjella.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video Mpya ‘Komesha’

Licha ya kuwa mgeni katika fani ya mziki wa Bongo, Anjella ameonyesha ustadi mkubwa kufikia sasa.

Ukiskiliza wimbo huu, unapata kufurahia ushahiri na ufundi wake na ni muda tu kabla hajapata umaarufu nje ya Afrika Mashariki.

Kwa sasa hii ni mojawapo ya ngoma Bongo huku kanda ya wimbo huu ikititarajiwa hivi karibuni.

Mdundo wa wimbo huu ulifanyiwa utayarishaji na Beat Boy kutoka Konde Musisic Worldwide.

Kufikia sasa, wimbo huu una watazamaji zaidi ya elfu arobaini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=nwoCHl7pO8M

Leave your comment