Harmonize Aanza Maandalizi ya Video Mpya ya Amapiano

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize ameanza maandalizi ya kanda ya wimbo wake wa Amapiano.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Huu ni wimbo ambao Harmonize aliuimba wakati wa kuzinduliwa kwa Anjella kama msanii wa lebo ya Konde music Worldwide.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Wimbo huu ambao haujaachiwa rasmi ulishabikiwa kwa ukubwa katika hafla ile ya Anjella na Harmonize akasema kuwa ni wimbo ambao utatikisa mitandao na vyombo vya habari kwa kucheza kazi hii mpya.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Kumi za Bongo Zilizoachiwa Mwezi Aprili 2021

Kutoka mtandao wa Instagram, Harmonize amaonekana akiwa katika location au maandhari ya kuandaa video ambayo inatarajiwa kwa ukubwa sana.

Kufuatia hilo, Harmonize alitangaza ujio wa albamu yake iitwayao “High shool” ambao alisema ni wa kuwafundisha watu kuhusu mziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano Mpya Zilizovuma Bongo Mwezi Aprili 2021

Hivi karibuni Harmonize aliondoka Tanzania na sasa yuko Nigeria na Country Wizzy na Ibraah kwa maandalizi ya albamu hio.

Vile vile, hatimaye msani Killy ataachia albamu yake mpya ambayo itakua kazi yake ya kwanza tangu kusainiwa katika lebo hiyo ya Harmonize miezi sita iliyopita.

Kwa sasa, Harmonize ni miongoni mwa wasanii kama vile Diamond Platnumz, Lavalava, Marioo, Dogo Janja miongoni mwa wengine wanaoazimia kuachia albamu zao ndani ya mwaka huu.

Albamu hiyo ya ‘High School’ itakuwa ya pili tangia Harmonize aanza kazi ya muziki. Albamu yake ya kwanza kwa jina ‘Afro East’ ilitoka mwaka wa 2020.

Leave your comment