Nyimbo Mpya: Video Tano Mpya Zilizovuma Bongo Mwezi Aprili 2021
29 April 2021
[Picha: Harmonize Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Wiki hii wanamziki hawakusazwa katika kuachia kazi mpya hivyo tunaangazia nyimbo tano zinazovuma bongo kwenye mtandao wa YouTube:
Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea
Harmonize ft Awilo Longomba na H baba
Hii ni kazi mpya sana ya Harmonize aliomshirikisha nguli wa mziki barani Afrika Awilo Longomba na mwenzake wa Tanzania Hbaba. Ni wimbo wa starehe na burudanai na ulikpokelewa kwa ukubwa kwa sasa video hii ina watazamaji zaidi ya milioni tano.
Baikoko - Mbosso
Huu ni wimbo wa Mbosso ambao umetamba kwa muda wa wiki tatu sana. Kwenye wimb huu, Diamond amemshirikisha Diamond Platnumz. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya Milioni sita.
Hayakuhusu - Ibraah
Katika wimbo huu Ibraah alionea kumchamba Rayvanny kuhusu ugomvi dhidi yake na Harmonize. Wawili hao walikuwa na mazozano kuhusu aliyekua mpenzi wa Harmonize Bi. Fridah Kajala na mwanawe Paula.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021
Vibaya - Harmonize
Katika kujaribu kuomba radhi na kuwaheshimisha akina dada ambao amaekua na uhusiano nao, Harmonize alichia wimbo huu ‘Vibaya. Kufikia sasa ni wimbo uliokubaliwa sana na mashabiki na watazamaji zaidi ya milioni moja huku kanda yake ikitarajiwa hivi karibuni.
Sere - Olakira ft Zuchu
Msanii Olakira kutoka Nigeria alimshirikisha Zuchu katika wimbo huu wa mapenzi. Olakira alifanya busara katika kumchagua Zuchu kwa wimbo huu. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki nane kwenye mtandao wa YouTube.
Leave your comment