Nyimbo Mpya: Anjella, Harmonize Wadondosha Video ya Wimbo Wao ‘Kama’

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii toka lebo ya Konde Music worldwide Anjella na Harmonize wameachia kanda ya wimbo wao ‘Kama’.

Katika wimbo huu wawili hawa wanaangazia hisia walizonazo kwa mtu wanaopenda.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Mchanganyiko wa rangi ya mavazi katika kanda hii ni nzuri huku nyekundu ikiwa ndio ilitumika kwa sana.

“Jeshi Sounds by Abbah (Konde Boy)Kwanza namuomba Mungu iwe kweli Nipate wa kunipenda anirithie kwa moyo niepushe na matapeli,wale wa kula na kwenda mi nmeumbwa na choyo…” aliimba Anjella.

Anjella anaomba kupata mpenzi ambaye hatamuhada wala kumvunja moyo. Vile vile anaazimia kupendwa hadi atakapopelekwa nyumbani kwa wazazi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

Harmonize naye anaingia kwa kusema kuwa uzuri wa mke ni tabia, huku sura na shepu ni vya kuchangia tu.

Katika kanda hii, Anjella na Harmonize wanajitokeza kama wapenzi katika hafla ya maonyesho ya mitindo.

Wawili hao wanaonyesha ubabe wao kupitia mikato tofauti kwenye kanda hii. Anjella kwa upande wake ameonyesha ufundi wake wa sauti na hata muonekano wa kudensi.

Anjella ameingia kwenye sanaa hiii kwa kishindo na sasa ni muda tu mashabiki wamkubali kwa ukubwa zaidi.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu zaidi. Kwenye mtandao wa YouTube umepata watazamaji zaidi ya laki moja.

https://www.youtube.com/watch?v=x95uTLI2jOc

Leave your comment