Nyimbo Mpya: Proffessor Jay Atamba na Wimbo Mpya ‘Utaniambia Nini’ [Video]

[Picha: Professor Jay  Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Aliyekuwa Mbunge nchini Tanzania na msanii tajika Joseph Haule almaarufu Professor Jay ameachia ngoma mpya kwa jina ‘Utaniambia Nini’.

Professor Jay anajulikana kama nguli wa mziki wa hip-hop nchini Tanzania na kurejea kwake umekua wa kishindo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video Yake Mpya ‘For You’

‘Utaniambia Nini’ ni  kazi yake ya kwanza tangu kurejea katika ulingo wa mziki baada ya miaka mitano kama mbunge wa Mikumi.

Awali Professor Jay, alishirikishwa katika wimbo wa Stamina kwa jina ‘Baba’ wimbo uliopokelewa vizuri sana hadi ukakubaliwa na aliyekuwa rais wa Muungano wa Tanzania marehemu Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Samia Suluhu Ashauri Serikali yake Kuzingatia Changamato za Wasanii

Katika Wimbo huu Professor Jay anaangazia safari yake ya mziki huku akiwakashifu wanamziki wa kisasa kwa majigambo yasiyo na msingi.

Proffessor Jay anawakosoa wasanii wasasa kutofanyia mziki dharau na kuwa ni ajira kwa watu wengine.

“Kwenye mziki nilinza kabla yako shahidi mama yako (Utaniambia nini), Kama bata nmekula zaidi yako acaha ngojera zako (Utaniambia nini)Kama ng’ambao tulitimba kitambo,kitambo kabla yako(Utaniambia nini)…”aliimba Proff Jay.

Vile vile, anadai apewe heshima zake katika mziki ama sivyo azichukue kwa lazima. Hivyo katika kuachia mziki huu Proffessor Jay anaendelea kudhihirisha ufundi wake katika mziki wa hip hop.

Wimbo huu ulifanyiwa maandalizi na producer Bin Laden wa Tongwe records na video hii kuelekezwa na mwanalizombe.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya elfu thelathini na moja muda mchache baada ya kudondoshwa.

https://www.youtube.com/watch?v=I2WN49sqQS4&ab_channel=ProfessorJay

Leave your comment