Nyimbo 5 za Injili Unazohitaji kwenye Orodha Yako ya Mziki wa Pasaka

[Picha: Information Guide Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wakati sherehe ya kufa na kufufuka kwake Yesu Kristo inapokaribia, leo tuanakuandalia orodha ya nyimbo tano za Injili unazofaa kuwa nazo wakati huu wa Pasaka.

Mimina - Kwaya ya Mtakatifu Kizito

Mimina ni miongoni mwa nyimbo bora za Kwaya Katoliki ya Mtakatifu Kizito . Katika wimbo huu wanakwaya hawa wanaangazia baraka na neema za mwenyezi Mungu katika maisha yetu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya za Injili 2021 [Video]

https://www.youtube.com/watch?v=AkM7bziJfaM&ab_channel=RAJOPRODUCTIONS

Wastahili sifa – Goodluck Gozbert

Huu ni wimbo wa kumuabudu mwenyezi Mungu na kumpa sifa kwa kutulinda bila ya kutuhukumu kwa yale tunayotenda. Gozbert katika ubunifu wake ameimba na bendi ambayo inakupa hamu ya kumuabudu aliyetuumba kwa moyo mkunjufu.

https://www.youtube.com/watch?v=vbUxS6nYSbI&ab_channel=GoodluckGozbert

Relax – Christina Shusho

Katika wimbo huu, Christina Shusho anampa binadamu fursa ya kumamini Mungu katika maisha. Relax ni wimbo wake Shusho  ambapo Anaimba juu ya ujasiri wake wa kuamini kwamba Mungu atatimiza ahadi zake kwa wakati wake.

https://www.youtube.com/watch?v=bm9oGxhtbic&ab_channel=ChristinaShusho

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Christina Shusho Aachia Video Mpya ‘Hesabu’

Nikumbushe wema wako – Angel Benard

Huu ni wimbo ambao unampa binadamu fursa ya kujisalimisha kwa Mungu haswa katika kutafuta majibu ya tatizo anazopitia kwa maisha yake. Angel anasisitiza kumtumainia Mungu katika nyakati zote bila ya kusita.

https://www.youtube.com/watch?v=OLHyg6UbHBM&ab_channel=AngelBenard

Mountain –Rose Muhando

Katika wimbo huu Rose Muhando anamsifu Mungu kwa kuwa chanzo chake cha nguvu. Kimsingi wimbo huo unahimiza binadamu kumkimbilia Mungu kwani yeye tu ndiye anayeweza kutupigania katika shida zote.

https://www.youtube.com/watch?v=0mShuCpzmsE&ab_channel=RoseMuhandoOfficial

Leave your comment