Zuchu Aweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwimbaji Zuchu kutoka lebo ya WCB Wasafi amefikia ‘Subscribers ’ milioni moja kwenye chaneli yake ya mtandao wa YouTube.

Kwa sasa Zuchu amekuwa mwimbaji wa kwanza wa kike Tanzania kufikia idadi hiyo ya Subscriptions kupitia chaneli yake kwenye mtandao huo ndani ya muda mfupi zaidi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso, Anjella Wang'aa Kwenye Nyimbo Tano Bora Wiki Hii

Vle vile kwenye mtandao huo wa YouTube, kazi zake Zuchu zimetazamwa zaidi ya mara milioni 140 mpaka sasa tangu alipoachia kazi yake ya kwanza Miezi 11 iliyopita.

Akielezea furaha yake kwa kuandikisha rekodi hii mpya, Zuchu amewashukuru mashabiki kwa kumkubali kwa kishindo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya Kwa Jina 'Yalah'

“1,000,000 subscribers asanteni sana kwa upendo huu uliopitiliza wa kuniwezesha kufika subscribes 1 million ndani ya miezi 11 .nina vingi vya kuwashukuru ila kwa leo history hii tulioweka ndo ya muhimu…” aliandika Zuchu

Kwingineko, Msanii wa Bongo Nandy amefikisha watazamaji milioni mia moja katika mtandao wa Youtube.

Nandy alijiunga na mtandao huo mwaka 2016 na amepata watazamaji wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.

Kazi hizo ni kama vile,Tamasha zake anazoenda, matukio ya kijamii anayoshiriki na utayarishaji wa video za nyimbo zake.

Nandy pia amepata kuwashukuru mashabiki kwa kutazama kazi zake.

“Views 100M+ on @youtube Haikua kazi rahisi, Nashukuru kwa Watu wote waliofanikishwa kupiga hatua hii kubwa katika mziki wangu.Huu ni Mwanzo mpya wa kupambana na kufika mbali zaidi na kupeperusha bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla…” aliandika Nandy.

Leave your comment