Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya Kwa Jina 'Yalah'

[Picha: Mzigo TV]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Mbosso ameachia video mpya kwa jina ‘Yalah’.

‘Yalah’ ni wimbo yenye maudhui ya mapenzi. Kwenye wimbo huu, Mbosso anaeleza kuwa mtu yeyote anaweza kupata mapenzi licha ya kule anakotoka, au kazi anayofanya.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

Video ya wimbo huu imepokelewa vizuri na ina watazamaji zaidi ya elfu mia saba kwenye mtandao wa YouTube.

Video hii iliandaliwa na Hascanah anayejulikana kwa umahiri wake kwenye sanaa ya kuanda video.

‘Yalah’ ni mojawapo ya nyimbo kwenye albamu yake Mbosso ‘Definition of Love’ alioachia hivi majuzi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Albamu yake Mpya ‘Definition of Love’

‘Defition of Love’ in albamu ya Mbosso ya kwanza tangia aingie kwenye lebo ya Wasafi miaka mitatu iliyopita.

Kwenye albamu hii kuna nyimbo kumi na mbili na mbili za ziada ambazo wanaziita ‘Bonus tracks; yaani zawadi ya mashabiki.

Mbosso amewashirikisha wasanii mbali mbali kwenye albamu hii, wakiwemo kutoka Tanzania ni; Diamond Platnumz, Rayvanny, Njenje wa Kilimanjaro Band, Darassa na Babalevo kisha Spice Diana wa Uganda alafu Liya na Mr Flavour wa Nigeria.

Nyimbo zilizo kwenye albamu hii ni kama vile; Kiss Me, Pakua Ft Rayvanny, Karibu ft Diamond, Kadada ft Darassa, Your Love ft Liya, Yes ft Spice Diana, Nipo Nae, Limevuja, Baikoko ft Diamond Platnumz, Yalah, Mselelekoh, Sakata ft Mr Flavor, Tulizana ft Njenje wa Kilimanjaro band na hatimaye Mtaalam.

Albamu hii ilifanywa kwa ubunifu wa producers S2kizzy, Lizer, Trone, Abbah Process, Abby Daddy, Kapipo, Nusdur Venum na Artin Pro.

Kufikia sasa, albamu hii imepokelewa vizuri na inapatikana katika mitandao ya kucheza mziki.

https://www.youtube.com/watch?v=ijm4CHvJdGw

Leave your comment